Picha: Maisha Ya Muhamad Ali

 Muhammad Ali alizaliwa na kupewa jina Cassius Marcellus Clay mjini Louisville, kentucky mnamo 17 Januari 1942. Alianza kucheza ndondi akiwa na umri wa miaka 12 na baadaye akaishia kushinda dhahabu katika uzani wa light-heavyweight Michezo ya Olimpiki ya Roma mwaka 1960.

 Cooper alimbwaga Ali raundi ya nne lakini Mmarekani Ali alitimiza ubashiri wake kwa kumshinda raundi ya tano mbele ya watazamani 55,000 uwanja wa Wembley.

Alidundwa na wataalamu wengi wa masumbwi kabla ya pambano hilo lakini Ali alicheza kwa ustadi mkubwa Miami na kumlazimisha Liston kusalimu amri kabla ya raundi ya sita. Ali alitawazwa bingwa wa dunia uzani wa heavyweight akiwa na umri wa miaka 22.

 Ali, alitangaza kujiunga na kundi la Nation of Islam na akaacha kutumia majina yake ya awali na kuwa Muhammad Ali baada ya pambano hilo dhidi ya Liston. Alitetea ubingwa wake dhidi ya Liston mjini Lewiston, Maine mwezi mei 1965.
Ali alishinda Liston baada ya kumpiga knock-out dakika ya kwanza ya raundi ya kwanza. Hadi wa leo, wengi wanaamini Liston aliuza pambano hilo, lakini Ali amesisitiza kwamba alishinda kwa njia safi.

 Ali alirejea London kupigana na Henry Cooper kwa mara ya pili Mei 1966 katika uwanja wa zamani wa Arsenal wa Highbury. Mashabikji wake Uingereza, ambao hawakuwa wamemtambua mara ya kwanza, walimshabikia sana.
 Angelo Dundee, anayeonekana hapa akifunga mikono ya Ali kabla yake kupambana na Cooper, alikuwa akimsaidia Ali tangu alipoanza kucheza ndondi.
Ali alimshinda Cooper baada ya raundi sita na kumuumiza vibaya karibu na jicho lake la kushoto. Baada ya kifo cha Cooper 2011, Ali alisema: "Nitamkosa sana rafikin yangu wa zamani - alikuwa mpiganaji hodari na mwanamume muungwana."
Baada ya kutetea taji lake tena mara nyingine dhidi ya Zora Folley, Ali alipokonywa taji lake baada ya kukataa kujiunga na jeshi la Marekani lililokuwa likipigana vita Vietnam. Ilikuwa ni miaka mitatu baadaye aliporejea ulingoni tena
 Ali alishindwa mara ya kwanza na bingwa mpya wa dunia Joe Frazier katika Madison Square Garden mwezi Machi 1971. Pambano hilo hujulikana tu kama "The Fight" yaani Pambano Lenyewe. Ilikuwa mara ya kwanza kwa mabingwa wawili wa dunia wa heavyweight ambao hawakuwa wameshindwa kukutana ulingoni.
 Ali alishinda marudio ya pambano hilo dhidi ya Frazier ingawa pambano lake linalosifika sana lilijiri baadaye 1974 alipopigana na George Foreman katika pambano linalojulikana kama "Rumble in the Jungle" maana yake "Mngurumo Msituni". Ali alikaa raundi nane za kwanza akiwa amejibanza kwenye kamba, mbinu aliyoiita 'rope-a-dope'.
 Lakini alichomoka raundi ya nane na kumwangusha Foreman kwa ngumi kali na kuwa mwanamume wa pili kutwaa tena ubingwa wa heavyweight, akiwa na umri wa miaka 32.
 Ali alimshinda Mwingereza Joe Bugner mjini Kuala Limpur, malysia Juni 1975. Miezi minne baadaye, Ali alipata ushindi mwingine dhidi ya hasimu wake mkuu Frazier katika pambano la 'Thrilla in Manila'. Ali baadaye alisema lilikuwa jambo la kukaribia kifo zaidi alilowahi kuhisi.
Baada ya kushindwa an Holmes, Ali alipigana pambano moja, dhidi ya Trevor Berbick ambapo alishindwa kabla ya kustaafu kabisa akiwa na umri wa miaka 40. Kuondoka kwake kuliacha pengo katika tasnia ya ndondi, lililojazwa tu na kufika kwa Mike Tyson katikati mwa miaka ya 1980

Atlanta pia, alipewa tena nishani yake ya dhahabu kutoka kwa Michezo ya Olimpiki ya 1960. Ali alidai aliirusha nishani yake ya kwanza Mto Ohio baada ya kukosa huduma kwenye mgahawa wa Wazungu pekee
 Wakati wa kufunga karne, Ali alijizolea sifa tele. Watazamaji wa BBC walimpigia kura kuwa Mchezaji Bora zaidi wa Karne, mwaka ambao bondia wa Uingereza Lennoz Lewis alishinda tuzo kuu.
 Binti yake Ali, laila alianza kucheza ndondi akwia na umri wa miaka 15 na akaanza kucheza ndondi ya kulipwa 1999 kabla ya kumshinda bintiye Frazier, jackie Frazier-Lyde mwaka 2001. Laila alishinda taji la super-middleweight mwaka 2002 kabla ya kustaafu 2007.
 Mwaka 2001, filamu kuhusu maisha ya Ali ilitolewa, Ali akiigizwa na Will Smith. Ali aliendelea kusifika kote duniani, licha ya afya yake kudorora.Ilikupita Hii?

NAIBU SPIKA DK AKSON TULIA AMEITAKA SERIKALI KUTOA TAMKO KUTOKANA NA MAUAJI YANAYOENDELEA


Post a Comment
Powered by Blogger.