Picha 8 Za Mchezaji Nguli Duniani Wa Brazil Pele Akipiga Mnada Medali Zake Zote.

Mwanasoko wa Brazil Pele.
Nyota wa soka kutoka Brazil, Pele, ameamua kupiga mnada medali zote alizoshinda na vitu vingine vyenye dhamani alivyopata wakati alipokuwa mchezaji nguli duniani .

Mnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London na unatarajiwa kukusanya mamilioni ya pesa.

Wataalamu wanasema huenda mnada huo ukawa ndio mkubwa zaidi wa vifaa vya michezo kuwahi kufanyika.

Medali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa wakati wa mnada huo.

Nyota huyo wa zamani amesema atatoa sehemu ya fedha zitakazo patikana kwa mashirika ya kutoa misaada na kuongeza kwamba angelipenda historia yake kufurahiwa na kuonyesha katika makaazi ya watu na makavazi kote duniani.
Pele ambaye alianza kuchezea Brazil mika 60 iliyopita anasalia kuwa mfungaji bora zaidi wa mabao nchini humo.

Post a Comment
Powered by Blogger.