“Kuna baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi wanakiuka miiko ya utumishi wao,tunapokea malalamiko ya watu kubabimbikiwa kesi, rushwa, kunyimwa haki mbalimbali.Natoa rai kwa watumishi wote wa jeshi la polisi, msishughulike na wanyonge,shughulikieni kutatua matatizo ya wanyonge ili wajivunie kuwa na jeshi la polisi rafiki kwa raia wake.” WhatsApp-Image-20160624 (4)
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba ameyasema hayo leo alipohudhuria sherehe ya kumaliza mafunzo ya Polisi na Uhamiaji Chuo cha Polisi Moshi (CCP) hii leo.
WhatsApp-Image-20160624 (3) WhatsApp-Image-20160624 (2) WhatsApp-Image-20160624 (1)