NI VITA YA URENO NA CROATIA EURO 16 BORA REKODI YAIBEBA URENO.Michuano ya Euro mwaka 2016 inaendelea leo katika hatua ya mtoano (16 bora), ambapo kunafanyika michezo mitatu katika viwanja vitatu tofauti.

Saa kumi jioni, Poland wanacheza na Uswisi, Wales na Ireland ya Kaskazini wanachuana saa 1 usiku, wakati Croatia na Ureno wanapambana vikali saa 4 usiku.

Tukiangazia mchezo kati ya Croatia na Ureno ambao utachezwa kunako dimba la Stade Bollaert-Delelis uliopo manispaa ya Lens.
Huu ni mchezo wa kusisimua ambao unazikutanisha timu ambazo zimeamaliza hatua ya makundi na rekodi tofauti kabisa. 
Croatia walimaliza kama vinara wa kundi D mbele ya Uhispania, Uturuki na Jamhuri ya Czech pamoja na kumaliza ubabe wa Uhispania kutofungwa mechi 14 mfululizo katika michuano ya Ulaya, wakati Ureno walimaliza nafasi ya tatu baada ya kutoka sare michezo yote na kuingia katika hatua hii kama mshindwa bora (best loser), kwenye kundi lililokuwa na timu za Austria, Iceland na Hungary.

Kwa upande wa Croatia, leo kiungo wao mahiri Luka Modric anaweza kurejea baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Ufaransa kutokana na majeraha ya nyonga yaliyokuwa yakimsumbua.
Kocha Ante Cacic bado hajafanya maamuzi kama amtumie mshambuliaji Mario Mandzukic au Nikola Kalinic, ambaye alifunga katika mchezo dhidi ya Uhispania.

Croatia watakuwa watakuwa na faida ya kuwa na mapumziko zaidi, lakini mshambulizi Nikola Kalinic, amekiri kwamba mchezo wa leo hautakuwa rahisi kutokana na uimara wa wapinzani wao.
“Pengine tungeweza kupata wapinzani rahisi zaidi ya Ureno katika hatua hii, lakini inatubidi kucheza kwa juhudi kama tulivyofanya kwenye hatua ya makundi, tuna nafasi kubwa ya kusonga mbele. Sisi ni moja ya timu bora katika michunao hii, na kwa uwezo mkubwa wa safu yetu ya kiungo, basi tuna nafasi kubwa ya kuibiuka na ushindi,” Kalinic amesema.

“Hii ni fursa adhimu kwa kizazi chetu katika historia ya taifa letu, na tutakumbukwa tu endapo tutafanya jambo kubwa hapa,” mshambuliaji huyo wa Fiorentina ameongeza.

Kocha wa Ureno Fernando Santos amesema kwamba kikosi chake kipo kamili na wachezaji wake wote wamefanya mazoezi jana tayari kwa mchezo wa leo.

Santos anaamini kwamba magoli mawili ya Cristiano Ronaldo katika mchezo dhidi ya Hungary Cristiano Ronaldo yatamuongezea kujiamini, vile vile amesisitiza kurekebisha mapungufu kwenye safu yake ya ulinzi yaliyosababisha kuruhusu magoli mengi katika mchezo uliopita.

“Katika hatua hii hakuna tena nafasi ya kufanya makosa ya kizembe. Lazima tuwe na uwiano mzuri kuanzia safu ya ulinzi mpaka ushambulaiji kwa sababu tunapokwenda kushambullia tunaancha mapengo mengi nyuma kama ulivyoona kwenye michezo yetu ya hatua ya makundi.” amesema Santos.

Beki wa kushoto Raphael Guerreiro amepona majeraha yake ya misuli yaliyokuwa yanamsumbua ambayo yalisababisha akose mchezo dhidi ya Hungary.

Rekodi ya mechi walizokutana
Croatia
Ureno


Post a Comment
Powered by Blogger.