New Music | Idd Aziz - Kiswahili

Unafahamu Kiswahili? Mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Idd Aziz kutoka nchini Kenya ameachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Kiswahili.’ Ukihusu lugha adhimu ya Kiswahili, wimbo huu maridhawa umedhamiriwa kuwaunganisha wapenzi wa muziki na wajuzi wa lugha hiyo duniani kote.

Idd anauelezea KISWAHILI, “Nilitaka kutengeneza wimbo ambao hautaishia kuwa mzuri tu lakini pia uwe na ujumbe mkubwa utakaodumu kwa vizazi vingi.  Nahisi kuwa wanamuziki wa Kenya wakati mwingine huchukulia poa lugha za nyumbani, hasa Kiswahili hivyo huu utatukumbusha maana mahsusi ya Kiswahili na tafsiri yake ya pekee.”

Ukiandikiwa na kuimbwa na  Idd Aziz, KISWAHILI umetayarishwa na Jesse wa Revive Media huku video yake ikiongozwa na Sync. Kwenye video yake, Idd anaigiza kama mwalimu wa shule ya msingi huku hadithi yake ikitupeleka darasani ambako kupitia wimbo, anawafundisha wanafunzi umuhimu wa kushika urithi wetu kwa kujifunza Kiswahili.

Vitabu mashuhuri vya Kiswahili vya mtaala wa Kenya vinaonekana kwenye video hii iliyoongozwa kwa umahiri mkubwa.

KISWAHILI ni wimbo halisi wa Kikenya wenye vionjo vya Afrika Mashariki. “ Wimbo na ujumbe wa wimbo huu vimeshiba. Naamini mtaupenda. Nitaendelea kuachia nyimbo nzuri za Kiswahili,” anasema Iddi.Download Now
Post a Comment
Powered by Blogger.