NASHINDWA KUELEWA.


NASHINDWA KUELEWA:
Sina mpangilio wa jinsi ya kuandika kwa sababu akili yangu nayo leo haiwazi kwa mpangilio.
Sijuwi nani nimlaumu, mwalimu aliyenifundisha "news writting" (samahani mwalimu Ally), au mwalimu aliyenifundisha lugha shule ya msingi ( R.I.P mwalimu Chingare) au nani hasa alaumiwe?
Labda jamii inayonitegemea kuihabarisha labda inataka sana na kunilazimisha niwape aina fulani ya habari ktk mfumo wa aina fulani pia.
Ujue nimejikuta nashindwa kujua habari ni nn eti, tena hata sijuwi athari ama hasi au chanya ya kile ninachotangaza au kuandika.
Bado nalilia kuwa muhimili wa nne wa dola mmh, samahani kwa hilo.
Halafu ninapofanya mahojiano siku hizi sijuwi hata lengo langu la kufanya hayo mahojiano ni lipi isitoshe eti nafanya mahojiano bila hata angalau kufanya ka"risechi" kidogo ili kujiridhisha au hata kunijengea uwezo basi wa kile ninachokihoji.
Tuache hayo, nimejikuta naandika na kutangaza kuhusu michezo lakini jamani nimegundua huku ndiyo hakufai kabisaaaa.
Ujue huku unatakiwa kujua angalau sheria za mchezo, utamaduni, athari za kijamii eh hata athari za.kisaikolojia.
Yaani kwa bahati mbaya ninatumika bila kujijua halafu nacheeeeka. Eti huku nako sitakiwi kuonyesha ushabiki, namwangalia Pedro Pinto nashindwa kuelewa amefikaje pale jamani mbona natamani kuifikia "levo" yake lkn nashindwa?
Loh! nataka niwe mchambuzi bna siku hizi dunia ni kama kijiji ni rahisi tu kujua kuwa Messi amekosa penalti halafu katangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa, kwani kusoma takwimu nako nitashindwa?
Nimeshauriwa kwamba kama naweza ku"kopi" makala za akina Garry Linecker mbona nitakuwa maarufu hv punde Voda na Tigo wakiniona nitapata udhamini wao mkono unakwenda kinywani.
Haaa! nimesahau mhariri wangu
‪#‎Jeff‬ Gemo alinishauri nijifunze kwanza "kimombo" ili angalau niweze kutafsiri baadhi ya mambo.
Tatizo wenye ujuzi wa haya mambo akina ‪#‎Samuel‬ Samuel wamekaa kimya hawaniambii ninapokosea sijuwi wanaona kama nawadharau? mh nitaendelea.


                         Imani k.Mbaga.
                          0717469593.
Post a Comment
Powered by Blogger.