MZEE MWENYE AKILI NYINGI ASIYEKUBALI KUISHI KWENYE UHALISIA.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger.
·
MZEE MWENYE AKILI NYINGI ASIYEKUBALI KUISHI KWENYE UHALISIA
Kocha Arsene Wenger ni mmoja kati ya makocha wenye majina makubwa nchini Uingereza kama siyo duniani kwa jumla.
Mwaka 1996 ,alipewa rasmi kibarua cha kuinoa klabu ya Arsenal na hadi sasa ameshaifanya kazi kwa miaka takribani 20.
Ndani ya uwanja amefanikiwa kunyakua mataji kadhaa ikiwemo kombe la FA Mara 6 na ubingwa wa ligi kuu Mara 3.
Ndani ya uwanja pia Mzee Wenger amefanikiwa kuanzisha aina ya utamaduni wa namna ya kucheza, ktk mfumo wowote watakaocheza uwe 4-1-4-1 au 4-2-3-1 nk Arsenal hupenda kumiliki zaidi mpira na kucheza mpira wa wazi namna fulani ya "tik-tak".
Nje ya uwanja mzee huyu amefanikiwa kujenga msingi imara ya kiuchumi na kuifanya Arsenal kuwa moja kati ya klabu bora kumi zenye uchumi kwenye nguvu na kipato kikubwa.
Ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Himarate "Emirates" ni moja kati ya miradi iliyofanikiwa chini ya uongozi wa Mzee Arsene Wenger.
Changamoto kubwa anayokutana nayo ni kushindwa kubeba ubingwa wa ligi kuu kwa miaka kumi na miwili sasa toka walipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2004. Hali ambayo imeibua hasira Kali miongoni mwa mashabiki ingawa siyo wote kiasi cha baadhi yao kususia kuingia uwanjani au kuingia na mabango yanayomtaka mzee Wenger aondoke kwenye timu hiyo.
Sina shaka kuwa hakuna anaetilia shaka uwezo wa mzee huyu ktk ufundishaji lkn pasipo mafanikio historia haiwezi kukutetea na kuachilia huruma juu yako.
Mzee Arsene Wenger ameshindwa kuruhusu ufahamu wake kuishi ktk wakati uliopo.
Mpira leo hii umegubikwa na matumizi makubwa ya fedha kuanzia kwenye usajili hadi malipo ya mishahara.
Miaka ile ambayo Mzee Wenger alichukua uongozi ilikuwa ni miaka ambayo vipaji, ufundi na mbinu viliongoza mpira lkn sasa fedha inatangulia vipaji, mbinu na ufundi.
Anglia fedha zinazotumika leo kununua wachezaji linganisha na miaka ile.
Unaposikia leo Eliachim Mangala ananunuliwa kwa zaidi ya pauni mil 30 najiuliza Jaap Stam angenunuliwa kwa pauni ngapi?
Hili inakuonyesha namna ambavyo fedha na soko vimebadilisha Kbs mwelekeo wa soka hv sasa.
Wenger anataka kubaki peke yake akiamini kuwa matumizi madogo ya fedha na ufundi msingi kwa kutumia vipaji pekee vinaweza kukuletea mafanikio.
Sera ya mishahara inayotumika Arsenal haiwavutii wachezaji nyota kujiunga na klabu hiyo.
Hata mfumo wa usajili hauna mwelekeo wa kuinufaisha klabu hiyo ndani ya uwanja kwa maana ya kubeba makombe.
Mfano ukiangalia viungo salio nao Arsenal wote ni viungo wachezeaji mpira utawspenda kwenye kushambulia utawachukia kwenye kukaba. Santiago Carzola, Mesuit Oil, Aaron Ramsey, Jack Wilshare na sasa Granit Xhaka, ni wachezaji wenye vipaji vya kiwango cha juu ktk kuchezea mpira (kampa, kampa tena) lkn wasipokuwa na mpira au timu ikielemewa hutawaona wala hutajua wanafanya nn.
Viungo kama Gilberto da Silva, Patrick Vieira, Edu au baadae kwa mali Mathieu Flamin alikuwa na kazi ngumu ya kuwasaidia walinzi ktk kukaba na kuunda kikosi cha ushindani.
Ili kupata aina ya wachezaji hao ni lazima kuvunja benki kufanya usajili na kubadilisha sera ya mishahara hili kuwavutia na kuwafanya wabaki pale Himarati.
Bado namuheshimu Mzee Arsene Wenger "Le Professeur" naamini ktk uwezo wake na bado ana mchango mkubwa ktk soka na maendeleo ya Arsenal ila kama hataruhusu akili zake zihame toka karne iliyopita na kufanya kazi karne hii basi makombe itakuwa ni hadithi ya kusadikika kwa wana Arsenal.        Imani K Mbaga
        0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.