MZAMBIA KUFURU YANGA.
HUWEZI kukosea ukiziita hizi ni kufuru za kimataifa, hii ni baada ya kubainika kuwa Mzambia, Obrey Chirwa, atavuna dola 168,000 (sh milioni 363.476) kama mshahara katika kipindi cha miaka miwili atakachokaa Jangwani kwa mujibu wa mkataba aliosaini.

Seetheafrica.com lina taarifa kuwa kwa mwezi Chirwa atakuwa anadaka dola 7,000 (sh milioni 15.14), mshahara ambao umeacha gumzo nchini Zimbabwe ambako straika huyo alikuwa anacheza katika klabu ya FC Platinum ambayo pia ilimtoa Donald Ngoma na Thaban Kamusoko.
  Chirwa mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga kwa dau la dola 100,000 (sh milioni 216.3) ambazo kwa mujibu wa taarifa kutoka Zimbabwe ziligawanywa na yeye kuingiza dola 30,000 (sh milioni 64.9) dau la kusaini na dola 70,000 (sh milioni 151.449) ikichukuliwa na klabu yake ya zamani ya FC Platinum.

Mbali na kudaka kiasi hicho cha dau la usajili, Chirwa pia ataingiza dola 7,000 kama mshahara wake kila mwezi dau ambalo ni zaidi ya shilingi milioni 15 za Tanzania kitu ambacho kinamaanisha kuwa katika miaka yake miwili (miezi 24) Jangwani atapokea jumla ya dola 168,000 sawa na shilingi milioni 363.4 ambazo kwa timu zenye wachezaji wa mafungu zinaweza kulipa wachezaji wote 11 katika kipindi hicho.

Mbali na kuvuta mkwanja huo, pia uongozi wa Yanga katika kuhakikisha mshambuliaji huyo anatimiza vyema majukumu yake, wamempangia nyumba yenye hadhi ya vyumba viwili kwa ajili ya kuishi na familia yake.

Msemaji wa Platinum FC, Chizo Chizondo, aliuambia mtandao wa timu hiyo kuwa usajili wa mchezaji huyo umevunja rekodi katika kipindi hiki na kuwafanya nyota wengine nchini humo kuhamasika kuja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mshambuliaji huyo tayari ameungana na wenzake nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na pambano la Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe litakalopigwa Juni 28 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na tayari leseni yake pia imetua nchini
Post a Comment
Powered by Blogger.