MWANAMUZIKI MAARUFU KUTOWEKA.

Mwanamuziki wa Nigeria Ado Daukaka.

Polisi kaskazini mashariki mwa Nigeria wanamtafuta mwanamuziki mmoja maarufu Ado Daukaka ambaye alitoweka siku ya Ijumaa.
Mwanamuziki huyo anaripotiwa kutoweka baada ya kutoa wimbo unaozungumzia kushindwa kwa majukumu na ufisadi miongoni mwa wabunge.
Wimbo mmoja unaojulikana kama Gyara kayanka au wacha tufanye mambo mazuri kwa lugha ya Hausa, unaangazia jinsi wanasiasa hutua ahadai ambazo hawazitimizi.
Mmoja wa wake zake aliiambiaBBC kuwa bwana Daukaka alitembelewa na watu wasiojulikana saa za asubuhi, siku ya Ijumaa na huo ndio wakati wa mwisho familia yake ilimuona.
Post a Comment
Powered by Blogger.