Msanii Wa Muziki Wa Kizazi Kipya Jolee Afungukia Stori Yake Ya Kutekwa

 Msanii Sabra Mathew maarufu kama Jolee anayeishi Mwenge/dar -es-salaam alisema kuwa mkasa huo ulimkuta siku ya jumanne tarehe 10-05 mwaka huu,majira ya saa 7 mchana nyumbani kwake na rafiki yake anayefahamika kwa jina la Diva kwenye mitandao ya kijamii [so
cial nertwork].
  Alifunguka kwa masikitiko makubwaalisema kuwa ''nilifahamiana naye huyu dada kwa muda mfupi kupitia instagram ndipo nashangaa siku  Diva alinipigia simu na kuniomba tuonane nikamkaribisha nyumbani muda huo,ilipofika saa tisa tulitoka na kwenda tabata ambapo tuliingia Suppermarket tukanunua juice na pombe''.
    Akiongeza kuhusiana na mkasa huo alidai kua juice hiyo ilichanganya na dawa aliposhuka kupima nguo Tabata ambapo alipokuwa wanarudi alijikuta akipoteza fahamu ndipo sikujua kitu gani kinaendelea hadi pale niliposhtuka najikuta mahali ambapo sipafahamu,
   Alisema ''Wakati tunarudi gafla baada ya kunywa ile juice nilijikuta napoteza fahamu ndipo niliposhtuka nikajikuta nipo sehemu ambayo siifahamu na nipo kwenye godoro,pembeni yangu alikuwepo kaka mmoja ndio akaniambia nipo bagamoyo,nikajikuta kila kitu nimepoteza na hata ufunguo wa nyumbani kwangu,yule kaka akanielekeza kwenye kituo cha mabasi nikwamweleza konda akanielewa ndipo nikafanikiwa kurudi nyumbani nikamuomba mama mwenye nyumba anipe ufunguo wangu wa akiba na kukuta kila kitu kikiwa.
  Kuhusina na swala hilo kuwa la kiusalama Jolee alifunguka kuwa ''nilienda kituo cha Polisi Mwenge ambapo walishauri nikafungue kesi bagamoyo ukizingatia kule sipafahamu vizuri nikaamua kuachana nayo ila kwakweli inaniuma sana''.
  Pia Jolee aliwashauri vijana na wasanii wenzake wawe makini na mitandao ya kijamii maana sio kila mtu ni mwema wengine hawana nia njema,''kinachoniuma zaidi ni kuwekewa madawa na kwenda kutupwa mahali ambapo sio salama kwangu nibora wangechukua kila kitu lakini waniache salama,
     ''Nawashauri vijana na wasanii wenzangu haswa wakike wawe makini na mitandao ya kijamii mana sio kila rafiki ni rafiki wa kweli wengne sio watu wazuri na pia wale ambao wanania mbaya katika mitandao waache maana sio vizuri kumfanyia mwenzako kitu kibaya.

     Jolee anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa Dua Yangu video ikiwa imeongozwa na Kwetu Studios unaweza kumpata instagram kama joleetz

ANGALIA VIDEO YAKE ( DUA YANGU ) HAPO CHINI

Post a Comment
Powered by Blogger.