MH.MABULA ASEMA WIZARA YA ARDHI KUBAINI TAASISI ZINAZODAIWA FIDIA NA WANANCHI.“Halmashauri za Wilaya, Taasisi na Maafisa Ardhi hawaruhusiwi kuchukua mashamba ya wananchi kabla hawajakamilisha utaratibu wa malipo ya fidia kwa wananchi hao, ili kuondokana na malimbikizo ya madeni ya fidia ambayo malipo yake huchukua muda mrefu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi, alisema Mhe. Mabula.
Aidha Mhe. Mabula amewataka wananchi wanaodai fidia kuwa wavumilivu wakati Wizara yake inaendelea kufanya upembuzi wa taasisi hizo ili ziweze kulipa fidia zote zinazodaiwa na wananchi.
Vilevile Wizara hiyo imetoa ramani za mitaa kwa wenyeviti wa mitaa wa Jiji la Dar es Salaam ili wenyeviti hao waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, kwa mfano maeneo ya wazi, na nini kijengwe katika maeneo yao kama vile nyumba fupi au ndefu, hoteli au chuo ili kuondokana na migogoro ya kubolewa nyumba kwa kujenga eneo lisiloruhusiwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.