MCHEZAJI WA KUMI NA MBILI NA NAFASI YAKE.

MCHEZAJI WA KUMI NA MBILI NA NAFASI YAKE.

Ukiingia "signal Iduna Park" uwanja wa nyumbani wa Borussia Dortmund, au "Anfield" uwanja wa nyumbani wa Liverpool lazima ukae kimya kwa mtikisiko wa kishindo cha mashabiki wa klabu hizo wakiipa "sapoti" timu yao bila kujali matokeo yatakuaje.

Upo msemo usemao nyumbani ni nyumbani hata ikiwa pangoni, raha ya kuwa nyumbani ni uenyeji ktk kila kitu.
Siku ya Jumanne Dar Young Africans watakuwa wenyeji wa Tp Mazembe toka DRC ktk mchezo wa pili kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi.


Yanga iliyopoteza mchezo wa kwanza ugenini mbele ya Mo Bejaia 1-0, inataka kuutumia uwanja wa nyumbani kutengeneza mazingira ya kuvuka hatua ya makundi kuelekea nusu fainali.


Baada ya maandalizi ya muda huko nchini Uturuki Yanga watacheza mchezo wa Jnne wakiwa 12 uwanjani na hapa nataka kumzungumzia mchezaji wa 12 na majukumu yake.


Mashabiki wa timu duniani kote hujulikana kama mchezaji wa 12 wakiwa wana athari ya moja kwa moja katika saikolojia ya wachezaji uwanjani.
Hakuna kitu kinachompa mchezaji nguvu kama kujua kuwa umati uliojaa uwanjani uko nyuma yake.


Moja kati ya makosa makubwa wanayofanya mashabiki wa Yanga ni kuonyesha wazi hisia zao pale wasiporidhika na tukio, kiwango au uwepo wa mchezaji fulani uwanjani na OSCAR JOSHUA ni mhanga wa moja kwa moja ktk hili.
Mchezaji anaekosea atiwe moyo kwa kushangiliwa au kupigiwa makofi.
Hakuna hujuma kubwa kwa timu kama hujuma ya kuzomea au kulaumu na kumfundisha au hata kushinikiza maamuzi kwa mchezaji awapo uwanjani.
Wengi wamekuwa wakishangaa kwanini Yanga hucheza vizuri sana wawapo nje ya uwanja wa taifa? licha ya kutopata matokeo mazuri. Jibu la hili ni kwamba wakiwa nje hucheza bila presha ya mashabiki bila kuzomewa au kelele za "piga mbeleee..." "acha kuzubaaa..." nk


Hatuwatendei haki wachezaji wanaotupa furaha na.kutufanya tuinue mabega mjini kila siku kwa kuwalipa matusi au kuwazomea.
Zile ngoma tunazoingia nazo uwanjani hazitakiwi kuzimwa hata kama tuko nyuma kwa magoli matatu.
Tunatakiwa kuonyesha kuwa hawa ndiyo mabingwa wetu na ndiyo wawakilishi wa nchi.


Shabiki wa kweli hutakiwi kuuawa kisaikolojia na wanaoizomea timu yako badala yake ni kuzifunika kelele zao kwa kushangilia na kuimba nyimbo za ushindi.
Tuwafanye wachezaji wetu waone umuhimu wa mchezo wa nyumbani na raha yake kwa kuwapa "sapoti" ya uhakika hata wanaposhindwa kutimiza matarajio yetu.


Umewahi kuona mashabiki wa Liverpool wakiimba "you will never walk alone" katika mechi waliyopigwa nyumbani? Hiyo ndiyo maana halisi ya mpenzi na shabiki wa kweli.
MSUVA na OSCAR wanatakiwa waonje raha ya kuwa na kundi kubwa la mashabiki walio nyuma yao ili kuwafanya wajisikie kuwa YANGA ndiyo nyumbani kwao.


Unapozomea ujue kuwa unaihujumu timu hivyo uache kuwanyooshea vidole wengine kwa kuihujumu timu.
Mwana Yanga jitambue kuwa wewe ni mchezaji wa 12, watoe hofu wachezaji wa timu yako pendwa kwa kuwashangilia dkk zote bila kujali matokeo
Kila la heri kwa wana Jangwani wote.


                   Imani K Mbaga  
                0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.