VIDEO | MBUNGE WA CHADEMA ASIMAMISHWA KUHUDHURIA BUNGE KWA KUSEMA UONGO.
Mbunge wa Viti Maalum
Chadema Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge
baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la Polisi nchini limenunua magari
777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni idadi ya magari inayopangwa
kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa Kamati ya Maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge huyu ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.

Kamati ya Maadili,haki na madaraka ya bunge, imeliomba Bunge kumsimamisha Mbunge wa Viti MaalumChadema Anathropia Theonista kutohudhuria vikao vitatu vya bunge baada ya kukiri kusema uongo kwamba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya MakaziWilliam Lukuvi alihusika kupora viwanja vya waathirika wa mafuriko Jijini Dares Salaam jambo ambalo sio kweli kwa kuwa kwa wakati huo Lukuvi alikuwa Waziriwa Nchi Ofisi ya Rais Sera Uratibu na Bunge.
Adhabu hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia Leo June 17 hadi 21 mwaka huu.
Adhabu hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia Leo June 17 hadi 21 mwaka huu.