MATOKEO YA EURO NA HII NDO TIMU YA KWANZA KUTINGA ROBO FAINALI NCHINI UFARANSA.

Michuano ya Euro imeendelea tena katika makundi A na B kulichezwa mechi tatu katika viwanja tofauti mechi ya mapema iliwakutanisha wababe wa Uingereza Russia na Slovakia na matokeo yake Slovakia wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali.
Mchezo pili ulikuwa kati ya Romania na Switzerland na mchezo huu timu hizi zimetoka sare ya 1-1.
Na mechi ya tatu ilikuwa kati ya wenyeji Ufaransa na Albania mchezo huu ulikuwa mgumu kwa wenyeji hadi mapumziko timu hizi zilienda bila bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji kufanya mabadiliko na walioingia walibadilisha matokeo Antonia Grienziman na Dimitri Payet aliipatia Ufaransa dakika za jioni na kwa matokeo haya Ufaransa wana pointi 6,Switzerland pointi 4,Romania pointi 1 na Albania haina pointi na kwa matokeo haya Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kuingia robo fainali.
Post a Comment
Powered by Blogger.