Matokeo Copa America Na Euro,Sanchez,Messi Moto Na Ronaldo Hoi Kwa Iceland.


Michuano ya Copa America nchini Marekani usiku wa leo ilikuwa kufunga pazia kwa hatua ya makundi hatimaye timu za kwenda robo fainali zimejulikana huku mechi mbili zimechezwa.
Mechi ya kwanza imechezwa saa 03:00 usiku kati ya mabingwa watetezi Chile ambao walikutana na Panama na matokeo Chile wametuinga robo fainali kwa ushindi wa mabao 4-2 mabao ya Chile yamefungwa na Alexis Sanchez aliyefunga mawili na Eduardo Vargas mawili na Panama yamefungwa kupitia kwa Miguel Camargo na Abdiel Arroyo Molinar.
Mchezo wa pili umeanza majira ya saa 05:00 Alfajiri uliwakutanisha Argentina na Bolivia huku Argentina wameendelea kushinda mechi zote za makundi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 wakicheza bila Lionel Messi aliyekuwa benchi mshambuliaji wa PSG alifunga mabao mawili Ezequiel Lavezzi na moja likifungwa na Victor Cuesta.
Na hizi ndo timu nane zilizofuzu hatua ya robo fainali Marekani,Ecuador,Chile,Venezuela,Argentina,Mexico,Peru na Colombia.
Nchini Ufaransa kundi F lilianza jana kwa mechi mbili zilichezwa mchezo wa kwanza ulikuwa majira ya saa moja kamili ambapo Austria wavimbiana na Hungary na matokeo Hungary wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuongoza kundi.
Mchezo wa pili ulikuwa ni Ureno na Iceland Cristiano Ronald ameshindwa kuibeba timu yake baada ya kubanwa mbavu na Iceland kwa kufungana bao 1-1 na Luis Nani alianza kuwapatia Ureno bao mnamo dakika ya 31 hadi mapumziko Ureno 1-0.
Kipindi cha pili Iceland walisawazisha bao hilo na kuwanyima ushindi ureno wake na mastar wao.
Post a Comment
Powered by Blogger.