Marufuku Ndege Yenye Maadili Ya Kiislamu Nchini Malaysia.

Shirika la ndege la Malaysia, Rayani Air, linalozingatia misingi ya dini ya kiislamu katika biashara zake, limepigwa marufuku na idara ya safari za ndege nchini humo baada ya ukaguzi kuonyesha halijakidhi viwango na vigezo vya kiusalama.
Rayani Air ilianzishwa Disemba ikinadi kuendeleza desturi za kiislamu katika huduma zao zote zikiwemo za chakula cha wateja, kutouza pombe na wafanyikazi wanaovalia nguo ndefu na hijab kwa wanawake.
Shirika hilo linamiliki ndege mbili aina ya Boeing na lina wafanyikazi wapatao 60, wakiwemo marubani 8 na ina ofisi katika kisiwa cha Langkawi na pia husafiri sana Kuala Lumpur na mji wa Kota Bahru.
Post a Comment
Powered by Blogger.