Mambo Kumi Usiyoyajua Kuhusu Mwanasoka Ricardo KakaHivi unamfahamu au unafahamu nini kuhusiana na Ricardo kaka? Basi wakati unafukiria mimi nakuletea yale mambo 10 usiyofahamu au unafahamu lakini umesahau kuhusiana na Ricaldo KAKA moja kati ya wachezaji wangu bora kabisa kuwahi kutokea duniani.
Ø KWANZA,Jina lake kamili anaitwa Ricardo Izecson Dos santos .Kaka yake  mkubwa aitwaye  Rodrigo alikuwa anshindwa kutamka jina la Ricardo kwahyo akawa anasema tu Kaka ni huu ndo mwanzo wa kuitwa Ricardo Izecson Dosantos leite Kaka.

Ø PILI,Ricardo kaka alizaliwa tarehe 22 April mwaka 1982 huko Gama katika mji mkuu wa Brazil Brasilia na mzee Bosco Izecson Pereirra Leite ambaye ni mhandisi na mbunifu wa majengo na madaraja  na bi Simone dos santos  ambaye ni mwalimu wa Somo la biolojia.Familia ya Ricaldo kaka ilikuwa inajiweza sana kifedha  tofauti na wachezaji wengine wa kibrazil kwahyo ilikuwa rahis sana kwa Kaka  kufanya shule zote mbili kwa wakati mmoja soka na shule ya kawaida na alipofikisha miaka nane familia yake iliamua kuhamia Sao Paulo na alinza kucheza soka akiwa na miaka nane tu kaika timu ya vijana ya Sao Paulo.

Ø TATU,Alipofikisha umri wa miaka 18 almanusura Ricardo kaka achane na kucheza soka baada ya kupata ajali mbaya ya kuvunjika uti wa mgongo lakini kutokana na familia yake kujiweza alipatiwa matibabu na kupona kabisa na mwenyeewe hakuamnini kama angecheza ten ampira lakini alirejea uwanjani na kila akifunga vidole hunyoosha juu akimshukuru mungu kwa aliyomtendea na sehemu ya mshahara wake ulienda kanisa la nyumbani kwao kama sehemu ya shukrani.

Ø NNE, Alianza kucheza  mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha Sao Paulo  msimu wa 2001na alikwenda kuwafungia magoli 58 katika michezo 118 Saulo Paulo  lakini katika msimu huo wakichukua ubingwa wao wa kwanza wa ligi.Mechi yake ya kwanza ya kaka katika timu ya taifa ya Brazil ilikuja tarehe 31 january mwaka 2002 dhidi ya Bolvia na kaka mpaka sasa kaichezea Brazil michezo 91 nakuingia kambani mara 29.

Ø TANO,uwezo mkubwa aliokuwa nao Ricaldo Kaka suala la kwenda Ulaya lilikuwa haliepukiki na timu kadha wa kadha zlitajwa lakini walikuwa AC MILAN wakitangaza kumsajili msimu wa 2003 kwa kitita cha paund mil 8.7 na mmiliki wa Ac Milan Silvio Belusconi akisema huyu kijana ni peanuts yani ni karanga na alikuja kuchukua pahala pa Rui Costa akicheza nyuma ya mdenish Joh dal tommason,Philipo pipo Inzagi na Adry shevichenko.Kaka  sio tu alikwenda kuichezea Ac Milan michezo 170 huku akifunga mara 70 lakini pia akishinda champions league kwa kuivuruga Liverpool mawilim kwa moja akitakata vilivyo kwenye kiungo ya Milan iliyokuwa na watu kama Marsimo Ambrosini Claerance Sedorf na Andreal Pirlo

Ø SITA,Msimu wa 2004 kaka alichaguliwa kuwa balozi wa UN akijihusisha zaidi na masula ya vita dhidi ya njaa na alipoulizwa sababu ya kukubali kazi hyo alisema sifanyim hii kazi kwasabau tu naweza kuifanya lakini naifanya kwasababu sisi wacheza soka tunalo jukumu kubwa kuwasaidia wasiojiweza.Lakini pia alishawahi kutokea kwenye cover ya video game ya FIFA ya 2007 akiwa na Ronaldinho Gaucho.

Ø Saba,Siku mbili kabla ya xmas yani tarehe 23 December 2005 Ricardo kaka alifunga ndoa na mpenzi wake wa utotoni bi Caroline Celico harusi ikihudhuriwa na watu 600 lakini kitu amabacho pengine kitakusisimua sana nikuwa mpaka Ricado kaka nakuja kuoa hakuwahi kukutana na mwanamke yeyote hapo  kabla yan alikuwa ni bikira dahh kumbe inawezekana jama.’’KAKA anasema watu wengi wanashangaa nlakini mimini mkristo na maheshimu taratibu”bi Caroline mwenyewe anasimulia akisema”siku ya kwanza tu nilipokutana naye air port anaraejea nyumbani nilijua kuwa alikuwa sahihi kwangu na wakati huo nilikuwa na miaka 14”nilimmwambia asaini uatgraphy yangu na rafiki yangu kwa rafiki yangu akaandika with love frpm Kaka lakini kwangu akaandika with kisess from kaka”

Ø NANE,Msimu wa 2007  sio tu alishinda tuzo ya mchezxaji bora wa Italia ikiwa ni  kwa mara mbili mfululizo lakini pia kaka alitajwa kuwa mchezjai bora wa dunia akipata kura 1047 akiwabwaga Lionel Messi aliyepata kura 504 na Cristiano Ronaldo aliyepata kura 426 akingia kwenye kikosi cha FIFA lakini pia akishinda paia tuzo ya chma cha wachezaji wakimataifa maaraufu kama FIFPRO.Na kwa taarifa yako  tu hyu ndo mchezaji pekee aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mbele ya Lionel MESSI na Cristiano Ronaldo.

Ø TISA,June 3 2009 manchster city ilisadakika kutoa kitita cha paund mil 100 kumhamisha Ricardo kaka lakini drector wa Ac Milan akasema ataruhusu ikiwa kaka na mancity watakubaliana masula binafsi hata hivyo june  30 ikaripotiwa Real Madrid kutoa kitita cha euro mil 68 kumnyakua hasa baada ya Florentino Perez kushinda tena kiti cha urais na june 30 Ricardo kaka akitangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Real Madrid.

Ø KUMI,Kaka hakuwa na wakati mzuri ndani ya kikosi cha Real Madrid kutokana na majeraha na kukosa nafsi mbele ya mesut ozil na kina Angel Dimaria lakini aliicheza Real Madrid michezo 85 nakufung amara 23 n msimu wa 2013 akarejea tena nyumbani sio Brazil bali AC Milan.kaka alicheza Milan msimu mmoja na kwenda zake marekani kujiunga na Olando City akicheza mechi 31 na kufunga mara 11 pekee kabla ya kutolewa kwa mkopo kurejea nyumbani sao Paulo anakocheza mpaka sasa .

Ø NB:Ricardo kaka anasema mchezaji wake ambae alikuwa anamtazama sana akiwa anakuwa ni  mchezaji wa zamani wa Sao paulo na PSG Raimundo Souza Vieira  de Oliveira alimaarufu kama Rai.mchezaji bora wa kizazi chake unyumbulifu,ubora wa miguu yake yote miwili na jicho la pasi  vilikufanya ukimtazama ukatamani kununua viatu vya soka akikufanya uhisi soka ni mchezo rahisi sana.
Ilikupita Hii Ya Mtoto Ambaye Alizaliwa Moyo Ukiwa Nje Ya Mwili Wake.

Post a Comment
Powered by Blogger.