MAAJABU YA HISTORIA BIBI HARUSI AMNYONYESHA MTOTO AKIFUNGA HARUSI,NA KUZUA GUMZO SOMA HAPA.

Katika harusi, vitu vingine ambavyo havitarajiwi hutokea na kuweka kumbukumbu ambayo baadae hugeuka na kuwa historia kubwa.
Mwanamke mmoja nchini Canada amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya picha yake akimnyonyesha mwanae wa miezi tisa wakati wa ibada ya harusi kusambaa.
Christina Torino-Benton, mwenye umri wa miaka 30, alisema kwamba mtoto wake huyo alianza kuliwa wakati akiwa ibadani kutokana na uchovu aliokuwa nao sababu ya maandalizi ya harusi siku moja kabla.
Ndipo alipoanza kumnyonyesha wakati mchungaji akiendelea kuzungumza na ndipo mpiga picha wake alipompiga picha hiyo.
“Wala sikuona shida mimi kumnyonyesha mwanangu” alisema mama “hicho ndicho kilikuwa kitu pekee cha kufanya kwa wakati huo”
Bibi harusi huyo ndiyo alikuwa wa kwanza kuweka picha hiyo katika mtandao wa Face book na kuandika ambapo zaidi ya watu 7000 wali “like” picha hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.