LEO ZAMU YA RONALDO PAMOJA NA REKODI ZA KUSISIMUA KATI YA HUNGARY NA URENO NANI YUPO JUU.Ureno leo wanakutana na Hungary kuwania nafasi ya kufuzu kuelekea hatua ya 16 bora katika mchezo wa kundi F utakaofanyika kunako dimba la Stade des Lumieres lililopo manispaa ya Lyon.
Kocha wa Hungary Bernd Storck anaweza kufanya ‘rotation’ katika kikosi chake kufuatia kujihakikishia nafasi ya kushiriki hatua ya 16 bora.
Hungary kwa mara nyingine tena watakuwa bila ya mchezaji wao Attila Fiola, ambaye ana majeraha ya kifundo cha mguu, hivyo beki wa kati Adam Lang atakuwa na jukumu la kuanza tena kama beki wa kulia.
Kocha wa Ureno Fernando Santos atasubiri ripoti ya daktari ili kujua kama ataweza kuwatumia beki wake wa kushoto Raphael Guerreiro na kiungo Andre Gomes – wote wakiuguza majeraha ya misuli.
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo anatarajia kucheza mechi ya 17 katika michuano ya Ulaya, akiweka rekodi mpya.
Hungary ni kama tayari wameshafuzu, ushindi ama sare ya aina yoyote katika mchezo wa leo utawahakikishia nafasi ya kwanza katika kundi F.
Ushindi kwa Ureno leo utawahakikishia nafasi ya kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano na watakuwa vinara wa kundi hilo vinginevyo Iceland nao washinde idadi kubwa ya mabao.
Kama Iceland na Portugal wote wakitoa sare, basi Iceland watamaliza nafasi ya pili labda ikitokea Ureno wawe na idadi nzuri ya mabao.
Mpaka sasa Ureno hawajawa na matokeo ya kuridhisha, sare mbili katika michezo yote ya awali. Wakipiga mashuti 49 na kufanikiwa kupata goli moja. Katika mashuti yote hayo, 19 yamepigwa nje ya lango, 15 yamelenga lango na mengine 15 yamezuiliwa. Hii inaweza kuwa hatari kwao endapo watafanya uzembe kwenye mchezo wa leo.
Akiwa amefunga magoli 364 katika michezo 348 na klabu yake ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ni mchezaji ambaye mara zote huwa na wastani mzuri wa kufunga – lakini ukame wake wa magoli katika michunao hii inaleta habari nyingine. Kati ya mashuti 20 aliyopiga katika michuano hii, manne tu yamelenga lango na hakuna lililofanikiwa kutinga wavuni.
Hungary hata wakipoteza mchezo wa leo bado wana nafasi ya kufuzu kwenda nafasi ya 16 bora kama ‘best loser’.
Kama wakishinda mchezo wa leo, basi wakutana na mshindi wa pili wa kundi E ambaye anaweza kuwa Ubelgiji, wakati ikiwa wakimaliza nafasi ya pili, maana yake watakutana na England. Na kama watamaliza ndani ya washindi watatu wa juu, basi watakutana na mshindi wa kundi C ambaye ni Ujerumani au kundi D. Hungary wameonesha kiwango kizuri mbele ya Austria na Iceland mpaka sasa, lakini kuanzia sasa kwenda mbele, mambo hayatakuwa rahisi kwa vijana hao wa Bernd Storck. Wanahitaji umakini mkubwa.

Takwimu za mechi walizokutana
Hungary
Ureno
Post a Comment
Powered by Blogger.