Leo Ni Kilimanjaro Star Vs Zanzibar Heros Ni Vita EURO 2016 Nchini Ufaransa,Je Unajua Kwanini Nimesema Hivyo Soma Hapa?


England vs Wales 1

Ndugu wawili England na Wales leo wanakutana katika muendelezo wa michuano ya Euro, mchezo wa kundi B utakaofanyika kunako dimba la Stade Felix Bollaert-Delelis lililopo manispaa ya Lens.

Wales wanaingia katika mchezo huu wakiwa kileleni mwa kundi baada ya kushinda mchezo wa awali kwa magoli 2-1 dhidi ya Slovakia, huku nyota wa timu hiyo Gareth Bale akirusha kijembe kwa England kwa kusema kwamba hakuna mchezaji wa timu hiyo angeweza kupata nafasi katika kikosi cha Wales.
Bales anaongeza kwa kusema kuwa wachezaji wa Wales wana moyo wa kujitolea zaidi kwa taifa lao kuliko wapinzani wao, kitu ambacho kocha wa England Roy Hodgson amekiita ni ‘kuwakosea heshima’.

Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey, vile vile amekazia kauli ya Bale kwa kudai kwamba timu yao ni nzuri na anamini ari waliyonayo ni sababu tosha ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao katika mchezo wa leo.
“Tumepambana sana kufika hapa. Sasa tunakula matunda yetu,” amesema Ramsey.
Tumekuwa pamoja wakati wa taabu na raha. Kila mmoja anapigania timu kuhakikisha tunafanikiwa.”

Kwa upande wake, Winga wa England Adam Lallana, ambaye alicheza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Russia ulioisha kwa sare ya bao 1-1 jijini Marseille, amewaasa wachezaji wenzake kutoyumbishwa na Bale na badala yake jicho lao watupie kwenye mchezo wenye huku akiwatahadharisha pia kumchunga Ramsey na mchezaji mwenza wa Liverpool Joe Allen.

“Ninafurahi sana kucheza na Joe Allen na najua namna gani ana kipaji kikubwa. Aaron Ramsey ni mtu mwingine mwenye kipaji cha aina yake, hivyo tusipoteze muda kumchunga Bale pekee na kusahau wachezaji wengine hatari,” Lallana amesema
“Kitu cha msingi ni kuheshimu timu yote kwa ujumla na kuangalia ubora wa udhaifu wao ili kujua namna gani ya kupambana nao.”

Mapambano ya uso kwa uso kati ya timu hizi mbili (Hea-to-head).
England
Wales
Post a Comment
Powered by Blogger.