KUTAMANI NI MWANZO WA KUMPENDA MTU?


NA MICHAEL MAURUS.

NDUGU wasomaji, karibuni sana katika safu hii ya uhusiano wa kimapenzi nitakuwa nikiwaletea kila Jumanne, ikiwa imeongezewa kionjo cha tungo ya wimbo wa Kiingereza na tafsiri yake.

Katika safu hii, mtindo wangu wa uwasilishaji wa mada ni tofauti na wachambuzi wengine wa mambo ya kimahusiano ambao huja na mada mezani na kusasambua kadri wanavyoona inafaa.

Kwa upande wangu, natumia njia shirikishi katika kuwasilisha mada zangu nikiamini wapo wasomaji waliowahi kukutwa na mikasa kadha wa kadha ya kimapenzi ambao wanaweza kutoa shuhuda ambazo mwisho wa siku, zitawasaidia wengi kuona ni vipi wenzao wamekabiliana na misukosuko iliyowahi kuwapata ndani ya mahusiano yao.
Mara ya mwisho niliwasilisha kwenu mada hii iliyokwenda kwa kichwa Unaweza kumpenda mtu siku ya kwanza kukutana naye?
Kama nilivyoahidi, leo ninawaletea maoni ya wasomaji wangu juu ya mada hiyo kama walivyonitumia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno, yaani sms.
Kama nilivyosema awali, neno nakupenda huwa ni rahisi sana kulitamka, lakini ni vigumu mno kuamini iwapo anayelitamka anamaanisha, yaani ni kweli anampenda kutoka moyoni anayemtamkia maneno hayo.
Kiuhalisia, wapo wanaochanganya maneno mawili, kupenda na kutamani. Kumpenda mtu ni tofauti kabisa na kumpenda.
Unaweza kuku mvulana anakutana na msichana kwa mara ya kwanza na kumtamkia kuwa anampenda na msichana huyo kuamini kwamba anapendwa kweli.
Hebu tuone wasomaji wa BINGWA wanasema nini juu ya nmada hii:
“Huwezi kukutana na mtu kutoka kusikojulikana papo hapo ukauruhusu moyo wako kumpenda, hiyo sio kupenda bali ni kumtamani na mapenzi ya namna hiyo hayawezi kuwa ya kudumu kwasababu zilikuwa ni tamaa za moyo, inatakiwa kama umempenda utafute muda ukae naye muongee msomane kwa muda mrefu ndio pendaneni. 0745826376
Huo utakuwa ni unafiki, kwani huwezi kumpenda mtu kwa siku moja wakati mmekutana kwenye daladala ama kituo cha daladala. Wenye tabia hiyo ni waongo tu.
Unaweza kumpenda mtu siku ya kwanza iwapo mmekubaliana pia ukaridhika naye. Warioba wa Bunda
Ni vigumu kumpenda mtu mara tu umwonapo mara ya kwanza ila utampenda baada ya kuwa karibu naye kwa muda mrefu ukifuatilia nyendo zake, hususan kitabia. Kamugisha wa Manispaa ya Kigoma.

Jinsi alivyoumbika, shape yake, mwendo wake, kutokana na vitru hiki hiki, naunga mkono, feruzi , siku ya kwanza unapata taharuki baada ya kubaini amekugusa, huwezi kumwam,bia nimekutaka, bbadaye unaweza kumweka wazi, nakuunga mkono. Feruzi, temeke sokota.
Mapenzi ni nini? Mapenzi ni pale tu macho ya wawili wenye jinsia mbili tofauti yanapogongana na mara moja kuibua hisia mpya ambazo ndizo hizo za mahaba. Hivyo, macho yanapoona, moyo hutamani, ni katika hatua ya kwanza kabla ya kumalizia kazi yake ya pili ambayo ni kupenda.

Kumbe sasa kiukweli mtu hutamani kwanza kabla ya kupenda kwasababu kupenda kunataka mazingira ya kutosha kujiridhisha kabla ya kutamka ‘nakupenda’.
Miezi mine na zaidi, mwaka na zaidi pia ni muda unaotosha kujipima kuwa upo kwenye tama ila isiwe chini ya mwezi mmoja, huku ukizingatia kuwa karibu sana na mwenzi wako ndani ya kipindi hicho cha mtazamo. Erick Ngula wa Iguguno, Singida.
Unaweza kumpenda mtu kwa dakika mara ya kwanza tu baada ya kuonana naye. Huo ni upendo wa nje na tena unaweza kumpenda mtu baada ya muda fulani, siku, mwezi au mwaka na baada ya hapo ukapenda. Huo ni upendo wa ndani na ndio wa kweli. Mshiriri Mbaga wa Moshi, Kilimanjaro.

Ni kweli huwezi kupenda kwa siku moja, vigezo vya tabia lazima kwa kuwa mmelelewa na kuishi mazingira tofauti. 0654143226.
Ni kweli huwezi kukutana na mtu ukampenda kwa muda huo huo. Jakline Chambal.
Kwa mtazamo wangu, kuna utofauti mkubwa sana kati ya kupenda na kutamani, kutamani ni ile hali ya kumuhitaji mwanamke kwajili ya kufanya naye mapenzi tu na kupenda ni kumfanya mtu awe wa maisha yako hata akikwambia kuwa hayupo tayari kufanya na wewe mapenzi mpaka mfunge ndoa unakuwa upo tayari , huko ndio kupenda. Lizwan Alfa wa Njombe.

Huwezi kupenda bila kutamani. Hayo ni maneno mawili ambayo yanategemeana, Tamanio huwa moyoni kabla ya matendo, ukitamani kuwa na jambo, kitu au mtu ukidhamiria kuwa nacho katika himaya yako, ndipo upendo unapoanza kutimia.

Pia upendo umegawanyika katika mambo haya-kuthamini, kujali na kutunza. Kutamani ni kama kunyenyekea, kuwa na hulka pamoja na dharau juu ya kitu hicho.

Chanzo Bingwa
Post a Comment
Powered by Blogger.