KUNA HUJUMA ZA KUTAKA KUNIFUNGIA JERRY MURO.

KUNA HUJUMA ZA KUTAKA KUNIFUNGIA JERRY MURO.

Nimepokea ujumbe mzito kutoka kwa raia mwema ndani ya shirikisho la mpira wa miguu nchini -TFF zikionyesha kuna kila dalili za KUNIFUNGIA kutoshiriki shughuli za mpira nchini. 

Moja ya sababu kubwa niliyoambiwa na raia mwema huyo ni kuwa nimekuwa nikiwapa wakati mgumu sana baadhi ya viongozi na watendaji wa TFF ambao wamekuwa wakipambana kurudisha nyuma mafanikio ya klabu ya Yanga.

 Nimepokea taarifa hizo kwa huzuni kubwa sana na kwa masikitiko na mpaka sasa sitaki kuamini kama naweza kuwa kikwazo kwa baadhi  ya watu ndani ya TFF.

 Kutokana na sababu hizo nimeamua kuweka mtego mmoja tu wa kusubiria hiyo barua inayoandaliwa na nikikabidhiwa rasmi tu NITAAMINI KWELI TAARIFA NILIZOPEWA NI ZA KWELI NA HUJUMA DHIDI YANGU NI KWELI. 

NAWAOMBA WANA YANGA NA MAMILIONI YA MASHABIKI WA SOKA TUWE WA TULIVU KWA SASA MPAKA HAPO WATAKAPONIKABIDHI BARUA KAMA NI KWELI ILI NA SISI TU WAJIBU KWA SAUTI YA UMOJA WETU.

 Imetolewa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano yanga. Jerry Cornel Muro 28/06/2016
Post a Comment
Powered by Blogger.