KINYONGA
MTUNZI; Dorcas Safiel
sehemu ya kwanza..
 KINYONGA


Hakika nilimuamini kupita kiasi kitu ambacho sikuwayi kufikiri kama ata kuja kuharibu ndoto zote za maisha yangu ata kwa yale niliyoyapanga tayari alifanikiwa kuyaharibu yote....


  
Jina langu ni Irene msichana niliyebarikiwa na kila kitu ambacho anastahili kuwa nacho mwanamke Miriam ni rafiki yangu ambaye nilikutana naye kipindi ninasoma chuo na yeye ndo aliyenikaribisha siku ya kwanza tu kuingia darasani alinipa tabasamu nzuri sana na karibu kama mgeni mpya wa darasa lao,unzuri wangu ulikuwa ni tishio kwa wingi kitu ambacho kilifanya wasichana karibia wote wa chuo wanichukue na kuogopa kutembea na mimi njiani kwa kuona kero yangu ya kuitwa ovyo na wanaume tofauti tofauti njiani,nilipenda usumbufu huo nakujiona mimi ni zaidi ya wote na kwa jinsi nilivyo ndivyo nilivyojiamini zaidi, wazazi wangu walifariki miaka michache iliyopita na nikawa nalelewa na mama yangu mdogo pamoja na mume wake na kipindi nilipo maliza sekondari baba yangu mdogo ndo alikuwa mwanaume wangu wa kwanza na kwa tendo hilo ata mama yangu mdogo hakufanikiwa kujua kwa usiri mkubwa na safari zake za kusafiri kwa muda mrefu zilisaidia kwa kipindi hicho.
Miriam ndiye peke yake nilimuamini na kumwambia siri hiyo kuwa mimi ninatembea na baba yangu mlezi,tuliendelea na maisha ya chuo mpaka mwaka wa pili nikapata mwanaume ambaye alinipenda sana tokea mwaka wa kwanza nilipoaza degree yangu pale chuoni lakini kwa nafsi yangu nilikuwa napenda na kutamani tu wanaume za watu kwa kujua nitapendwa zaidi kuliko mwenye mali yake lakini nilipomzungusha johnson vya kutosha mwaka mzima na miezi nikajua ndiye atakuwa kama wakuzugia kwangu huku penzi lote likiwa kwa wanaume za watu hasa baba yangu,siku niliyomwambia johnson kuwa nimekubali kuwa nawe basi alifurahi na mchana alinitoa lunch na akanipa 100,000 kama nauli sikuamini macho yangu kama kusema ndiyo tu anaweza kunipa hela yote hiyo na kuingia gharama ya kulipia bill ya chakula kiukweli nilikuwa na wanaume 3 lakini hakuna ata mmoja wao ambaye niliaza naye mahusiano akanipa hela yoyote zaidi ya kiss na asante.
Nilimwambia miriam kwa siku inayofuata nilipokutana naye chuo kuwa johnson nimemkubali na cha kushangaza kanipa laki kama asante kwa kukubali ombi lake kuu kabla miriam yakujibu nilimuona johnson anakuja sehemu tuliyokaa akiwa na begi lake na vigrass viwili mkononi nikamwambia miriam eenh!! johnii yule anakuja miriam alijeuka na kumtazama na johnson alikuwa amefika tulipokaa na kusalimu 'mambo zenu' tuliitikia na miriam akaomba atupishe lakini kabla yakuondoka kwake nilimtambulisha kuwa huyu ndo shemu wako kwahiyo nichungie ukimuona mtu yuko naye niambie huku nikimalizia kucheka,tulipiga story za maisha na kusoma kwani wote tulikuwa darasa moja alinipa juice nakuniambia ananipenda sana naomba kama natatizo lolote nimwambie muda wa darasani ulifika natukasoma nakuondoka home.
 Miezi michache ikapita katika mahusiano yetu nikawa naona mabadiliko kwangu mwenyewe na pamoja na kwa miriam kwangu nilikuwa nahisi kumpenda sana johnson nakumuonea wivu ata akisimama na msichana nahisi atamtongoza lakini kwa miriam nilikuwa naona kama upendo kwangu umepungua na anapenda sana kufuatilia mahusiano yetu mimi na johnson lakini ata hivyo niliaza kupunguza mapenzi kwa wanaume wote ata baba yangu alishutuka juu ya hilo na aliponiuliza nilimwambia  kuwa niko busy na shule kwahiyo anipe muda. Sikumpenda johnson kwa pesa zake nahisi kwani kuna kipindi alipitia maisha magumu lakini bado nilisimama naye pamoja ....Mwaka wa mwisho wa kumaliza chuo ndio nilikuwa nasoma sana ili nisifail na kwa akili tu nilipewa zawadi na mwenyezi mungu tulifanya mitihani lakini miriam alikuwa kama hana raha nami ata mpenzi wangu naye aliliona swala hilo nakuhoji mara kadhaa lakini hakukuwa na jinsi tukamaliza chuo...ikawa nikusubiri matokeo na ajira tu huku mapenzi yakiwa moto moto!!!.....


ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI YA IRENE UONE NINI KILITOKEA KATIKA MAISHA YAKE..
Post a Comment
Powered by Blogger.