Je Wajua Hii? Msanii Nuh Mziwanda Kuhusu:Jike Shupa Na Video Queen.
Msanii Nuh Mziwanda.
MSANII Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, amesema kuwa wimbo wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba amemwimbia mpenzi wake wa zamani, Zuwena Mohammed ‘Shilole.

Nuh Mziwanda ambaye alikuwa mpenzi wa Shilole mpaka kufikia hatua ya kuchora tattoo ya jina la msanii huyo alisema mahusiano yake yalitawaliwa na mateso, wivu uliokithiri pamoja na kichapo.
“Nikisema nielezee mapenzi yangu niliyopita muda mwingine nasikia uchungu sana ila yalijaa tabu za kila aina ikiwemo mateso, wivu na  kichapo,” alisema.

Alipoulizwa kwanini aliamua kumtafuta ‘video queen’ anayefanana na Shilole alisema:  “Wimbo huo ulimlenga ex wangu, hivyo nililazimika kumtumia msichana anayefanana copyright na Shilole,” alisema.
Post a Comment
Powered by Blogger.