Kampuni Ya Microsoft Yaanza Biashara Ya Kuuza Bangi


Kampuni ya Microsoft imeingia kwenye orodha ya makampuni yaliyojiunga na biashara ya kuuza bangi katika majimbo ya nchini Marekani ambako inaruhusiwa kwa mujibu wa sheria za majimbo hayo.
Kampuni hiyo imeungana na kampuni nyingine "Kind Financial - inayotengeneza programu za kusaidia wadhibiti kufuatilia uzalishaji na mauzo ya bangi.
Majimbo kadhaa nchini Marekani yameruhusu uuzaji wa bangi kwa matumizi ya kimatibabu na kujistarehesha, japobangi ni haramu chini ya sheria kuu za nchi hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.