JIPYA LAIBUKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI.


hospitali ya muhimbili
Na Dorcas Safiel
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii,jinsia, wazee na watoto mh.Ummy Mwalimu amewataka uongozi wa hospitali ya Muhimbili kutoa maelezo juu ya uuzwaji wa dawa za magonjwa maalum kama kifua kikuu na ukimwi,alitoa agizo hilo bungeni na kuongezea ufafanuzi uliotolewa na naibu waziri mh.Hamis Kigwangala kufuatia kwa taarifa kuwa dawa zinazotolewa bure kwa magonjwa mbalimbali zinauzwa katika hospitali hiyo pia ameahidi kurejesha mrejesho huo bungeni.
 Wakati huohuo hospitali ya Muhimbili kuanzia julai mosi mwaka huu itaaza kutoa huduma ya chakula bure kwa wagonjwa wote watakaolazwa katika hospitali hiyo yamebainishwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano muhimbili bw.Emelie Eligaisha na kusema hospitali inataka kujikita katika kushauri,kuchunguza na kutibu pili  hospitali inataka kuwaondolea hadha ndugu wa wagonjwa kwa kuingia gharama kubwa ya usafiri kwa kwenda hospital kila siku ata hivyo aliongeza kuwa mgonjwa atabidi kuchangia shilingi elfu hamisi kwa ajili ya kumuona daktari, gharama ya kulazwa na chakula.
 Pia muda wa kuona ndugu mchana kufutwa hivyo kulazimika kuona ndugu asubuhi saa kumi na mbili hadi sa moja na saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni.
Post a Comment
Powered by Blogger.