JE,UNAUJUA UGONJWA UNAOTESA WATU WENGI? SOMA HAPA;

Ugonjwa wa Bawasiri.Na;Dorcas Safiel, Alex Sonna

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU.

 JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI?! ~

Yamkini umesumbuka na tatizo hili na hujui nini cha kufanya au hujajua wapi upate suluhisho lako kwanza kabisa lazima ujue bawasili ni nini ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na je ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka \kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kusababisha kutoka kinyama au uvimbe sehemu husika..  watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huu ambao unawafanya kuwa na uoga wa kuelezea kwa watu ili kupata msaada au kwenda hospitali kupata tiba.

UMRI WA KUPATA UGONJWA HUU.

tatizo hili halina umri maalum wa kumpata mtu huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30-50. 

AINA ZA BAWASIRI.

Kuna Aina mbili za bawasiri

 BAWASIRI YA NDANI ~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili,aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa.

Aina hii imegawanyika katika madaraja manne 

 DARAJA LA KWANZA ;Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika.

DARAJA LA PILI ;hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.

DARAJA LA TATU ;hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.

DARAJA LA NNE ;hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

BAWASIRI YA NJE ~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kusababisha kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu la haja kubwa pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS.

CHANZO CHA TATIZO.

chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni kama zifuatazo;

kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Tatizo la kutopata choo.

Kuharisha kwa muda mrefu.

Matatizo ya umri.

Kukaa kitako kwa muda mrefu.

Uzito kupita kiasi.

Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu. 

DALILI ZAKE NI;

 Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa.

 kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia.

kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa.

kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo.

kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana.

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKANA NA BAWASIRI.

matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia.

Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia 

kula mboga mboga za majani.

kula matunda.

kula nafaka zisizokobolewa.

Kunywa maji mengi anagalau grass 6\12 kwa siku.

Epuka kukaa chooni kwa muda mrefu.

 MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI 

 Kupata upungufu wa damu (anemia).

 Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo.

Hupunguza nguvu za kiume.

Huondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Kuathirika kisaikolojia 

Kukosa moral ya kufanya Kazi

 KWA MAWASILIANO ZAIDI;0717035770 AU 0753692612

TUPO MWENGE MPAKANI KARIBU NA BODI YA MIKOPO

 

Post a Comment
Powered by Blogger.