Je Ni Taifa Star Au Misri Uwanja Wa Taifa Leo?

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa star leo kitashuka uwanjani kucheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua ya kufuzu mataifa ya Afrika[AFCON] yatakayofanyika nchini Gabon mwakani.
Nahodha Samatta.
Mshambuliaji wa Genk na nahodha wa timu ya Tanzania Mbwana Ally Samatta leo atakiongoza kikosi katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kutafuta nafsi ya kucheza mwakani huku Tanzania wakiwa wanashika nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo kwani Misri wanaongoza wakiwa na pointi 7 hivyo wanahitaji sare ili waweze kufuzu huku Star ikihitaji ushindi wa aina yoyote.\
Mchezo huu ni muhimu kwa Star ili iweze kufufua matumaini ya kusonga mbele hivyo mechi hii itakuwa na upinzani mkubwa.

Post a Comment
Powered by Blogger.