HUZUNI YA UINGEREZA KWA MBUNGE WA LEBA KUUAWA NA KUMBUKUMBU YA MATUKIO NCHINI TANZANIA.

Mbunge aliyeuawa Jo Cox.
Ilikuwa siku ya Alhamis tarehe 16 mwezi huu wa sita ya huzuni kwa Waingereza na pigo kwa chama cha Leba ambapo mwanamama au mwanasiasa aliyekuwa kipenzi cha watu mwenye tabasamu kila wakati alipovamiwa na mtu asiyejulikana.


Huyu ni mbunge wa chama cha Leba cha  Ungereza Bi. Jo Cox ameaga dunia baada ya kupigwa risasi na kuchomwa kisu akiwa kwenye mkutano katika eneo lake la ubunge kaskazini mwa uingereza.

Katika historia kwa Waingereza na kubaki na kumbukumbu  ya kusema kuwa Jo Cox ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini humo tangu Ian Gow auawe mwaka 1990 ambaye aliuawa naye kwa kupingwa risasi na watu wasiojulikana.
Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana hata hivyo maswali mengi yanabaki kwa Ulimwengu kuwa huyu mwanaume aliyetenda kitendo hicho cha mauaji alikuwa na malengo gani kwa mwanasiasa huyu mpaka kumvamia na kumchoma kisu.
Penye ajali hapakosi mashuhuda ambao  wanasema kuwa mbunge huyo aliingilia kati mzozo kati ya yeye na wanaume wawili eneo ambapo alikuwa akikutana na watu katika jimbo lake.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema risasi ilifyatuliwa wakati Bi Cox aliingilia kati wakati anaingilia kati muuaji alichomoa kisu na kuanza kumchoma huku akiwa chini amelala huu ni mwendelezo wa matukio Duniani kote ambapo kila kukicha mauaji yameshamili kila kona.
Hili tukio hata kwetu hapa Tanzania limetokea katika maeneo mengi walio na kumbukumbu ni jijini Dar maeneo ya Kawe kijana mmoja alimchinja mpenzi wake pamoja na mtoto wake,kule Mwanza mauaji ya Watu waliovamiwa wakati wakiwa Msikitini pamoja na Watu nane kuvamiwa na kuchinjwa katika jiji la Tanga je ni kwanini matukio mengi yameendelea kuutesa Ulimwengu hata Marekani Watu zaidi ya 50 wameua kwa kuvamiwa na mtu mmoja aliyekuwa na Silaha kali huku Magaidi nao wakiendelea na juhudi zao za kuwatesa wasio na hatia na kusababisha watu wengi kuishi kwa kutangatanga kwa hofu za mauaji.
Post a Comment
Powered by Blogger.