Huyu Hapa Aliyewaua Wanawake 10 Ahukumiwa Kifo.


Jopo la waamuzi mjini Los Angeles, limeamua kuwa mshukiwa mmoja ambaye alipatikana na hatia ya mauaji, anayefahamika kama 'Grim Sleeper', anapaswa kuhukumiwa kifo.
Lonnie David Franklin Junior alipatikana na hatia mwezi uliopita, ya kuwaua wanawake tisa na msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mitano katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita.
Franklin junior alifahamika kama Grim Sleeper kwa sababu alitekeleza mauaji mengine baada ya miaka kumi na mitatu.
Aliwalenga wanawake masikini na wasichana wachanga ambao aliwaua na kutupa miili yao kwenye pipa za taka na mitaro ya kupitishia maji machafu.
Mshukiwa huyo sasa atakabithiwa hukumu yake agosti mwaka huu.

Post a Comment
Powered by Blogger.