HIZI HAPA TETEZI ZA SOKA ZA USAJILI BARANI ULAYA ALHAMSI YA LEO.


TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 30.06.2016.

Arsenal wana uhakika meneja wake Arsene Wenger, 66, atakataa dau lolote kutoka chama cha soka cha England, FA, ambacho kinamtaka achukue nafasi ya Roy Hodgson kuwa meneja wa England (Sun),


 Laurent Blanc ambaye ameondoka PSG wiki hii, pia anatajwa kuwania kazi ya kuifundisha England (Mirror),

 Vilevile meneja wa zamani wa Chelsea na Brazil, Luiz Filipe Scolari, 67, pia anataka kufikiriwa kupewa kazi hiyo ambayo aliikataa miaka kumi iliyopita (Daily Mail),

 Tottenham na Leicester ni miongoni mwa timu za EPL zinazomtaka beki wa Iceland Ragnar Sigurdsson, 30, anayechezea FC Krasnodar ya Urusi (Guardian),

 Pep Guardiola atafahamu siku ya Ijumaa iwapo Manchester City wamefanikiwa kumsajili mshambuliaji kutoka Colombia Marlos Moreno, 19, kutoka Atletico Nacional (Manchester Evening News),

 Real Madrid wanataka kumsajili kiungo wa Ufaransa na Leicester City N’Golo Kante, 25 (Marca].
 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekataa kusema kama hatoendelea kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lyon, Alexandre Lacazette, 25 (Canal+),

 Raheem Sterling ameshutumiwa vikali na mashabiki wenye hasira baada ya kuonesha video ya jumba lake la kifahari pamoja na sinki maridadi la kuogea, muda mfupi baada ya kurejea na kikosi cha England baada ya kutolewa kwenye Euro 2016 (Sun).

 Ryan Giggs anakaribia kuondoka Manchester United baada ya miaka 29. Winga huyo wa zamani, 42, amekataa kazi ya ukocha wa ngazi ya chini, chini ya meneja mpya Jose Mourinho (Daily Mail].

 Liverpool wamewaambia Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni 30 kumsajili Christian Benteke, 25 (Telegraph).

 Manchester City huenda wakabadilishana na Everton kwa kuwapa Wilfried Bony, 27, ili wampate John Stones, 22, na ikiwa Everton watamuuza Romelu Lukaku (Sun).

 Real Madrid huenda wakatoa dau la pauni milioni 75 kumtaka nyota wa Ubelgiji na Chelsea Eden Hazard, 25, kwa kuwapa Alvaro Morata, 23, pamoja na pauni milioni 40 juu yake (Mirror).

 Napoli huenda wakamsajili mshambuliaji wa Monaco kutoka Colombia, Radamel Falcao, 30, baada ya Gonzalo Higuain, 28, kusema anataka kuondoka (La Gazzetta dello Sport).

 Chelsea watatupilia mbali mipango ya kumrejesha Darajani Romelu Lukaku, 23, baada ya kukaribia kukamilisha uhamisho wa Michy Batshuayi, 22, kutoka Marseille kwa pauni milioni 33.2 (Daily Star).

Beki kutoka Slovakia Martin Skirtel, 31, huenda akakamilisha uhamisho wake kutoka Liverpool kwenda Fernabahce wiki hii (AMK Spor).

 Mchezaji wa kimataifa kutoka Japan Takuma Asano, 21, ameuliziwa na Arsenal (Express).

 Mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van Persie, 32, huenda akauzwa na Fernabahce, mwaka mmoja tu baada ya kujiunga nao akitokea Manchester United (Manchester Evening News).

 Newcastle wanakaribia kumsajili Dwight Gayle, 25, kutoka Crystal Palace, na Matt Ritchie kutoka Bournemouth. Winga Andros Townsend, 24, ataondoka St James’ Park, huku Crystal Palace wakitaka kutoa Pauni milioni 13 kumsajili (Daily Star). 
www.seetheafrica.com
Post a Comment
Powered by Blogger.