HIZI HAPA TETEZI ZA SOKA ZA USAJILI BARANI ULAYA SIKU YA JUMATATU.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 20.06.2016.

Manchester City wamepanda dau la pauni milioni 16.7 kumtaka Mshambuliaji wa Palmeiras Gabriel Jesus. Barcelona na Juventus pia wanamtaka chipukizi huyo, 19 (One World Sports).
Wakala wa Zlatan Ibrahimovic anasema mshambuliaji huyo wa Sweden hajaamua kama anataka kujiunga na Manchester United.(TF1 - in French).
wakuu wa United wanatarajia Ryan Giggs kutangaza kuwa anaondoka siku chache zijazo (Mirror).


Juventus wamemwambia Kiungo Paul Pogba anaweza kuondoka iwapo bei yake itafikiwa. Hueda akasajiliwa na Real Madrid badala ya Manchester City au Manchester United. (Marca)
N'Golo Kante pia ananyatiwa na Real Madrid (AS).
Leicester wana uhakika wa kumpata kiungo wa Nice Nampalys Mendy baada ya dau la pauni milioni 10 kukubaliwa. West Ham pia wanamtaka (Leicester Mercury)
Tottenham watakuwa na mazungumzo zaidi na Southampton kukamilisha usajili wa kiungo Victor Wanyama, 24. (Daily Mail)
Southampton wanamtaka kipa wa zamani wa Italia ambaye ni meneja wa zamani wa Sampdoria Walter Zenga, 56, kuwa meneja mpya (Sun)
Meneja mpya wa Aston Villa Roberto di Matteo anataka kumsajili kipa wa Watford Costel Pantilimon, 29, Lakini kuna utata kuhusu mshahara wake (Mirror).


Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 26, anatarajiwa kurejea Emirates baada kucheza kwa mkopo Roma ambapo mazungumzo ya kuongeza mkataba yanasuasua (Guardian)
Real Madrid wamewaambia Man United kuwa hawatomsajili kipa David de Gea, 25.(Express)
United wanamtaka beki wa Juventus Leonardo Bonucci, ingawa meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte angependa kumsajili.(Star) Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Post a Comment
Powered by Blogger.