Hizi HAPA TETEZI ZA SOKA ZA USAJILI ULAYA JUMATATU YA LEO.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 13.06.2016
Manchester United wapo tayari kutoa pauni milioni 79 kumsajili kiungo wa Paris St-Germain, Marco Verratti (Corriere dello Sport, via Daily Star),

 Zlatan Ibrahimovic ameahidi kutaja klabu anayokwenda "hivi karibuni" huku tetesi zikiendelea kuashiria kuwa ni Old Trafford (Daily Express),
 Pep Guardiola anataka kuwasajili John Stones, 22, wa Everton na Aymeric Laporte, 22, katika uhamisho utakaogharimu takriban pauni milioni 85 (Manchester Evening News), 
Liverpool wametoa pauni milioni 9.5 kumtaka kiungo wa Udinese Piotr Zielinski, 22 (Guardian),
 Liverpool wanapanga kumfuatilia beki wa River Plate Gabriel Mercado, baada ya meneja Jurgen Klopp kumtazama mchezaji huyo akiichezea Argentina kwenye michuano ya Copa America (Sunday People), 

Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Southampton, Victor Wanyama kwa pauni milioni 12 (Daily Star), Ronald Koeman anataka kumsajili kipa wa Southampton Fraser Foster mara atakapothibitishwa kuwa meneja mpya wa Everton, Sunday Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.