Hizi Hapa Sababu Za Lemonade Ya Beyonce KushitakiwaAlbamu mpya ya Lemonade iliotolewa na Beyonce Knowles imeorodheshwa miongoni mwa albamu zilizopendwa sana baada ya kutolewa mwaka huu,lakini ,kipande cha albamu hiyo kilichotolewa wiki moja kabla ya uwepo wa albamu hiyo kufichwa hadi wakati wa toleo la filamu fupi lililoandamana na albamu hiyo kimezua utata.
Kipande hicho cha albamu hiyo kilishirikisha msururu wa vipande vifupi vifupi vya albamu hiyo bila maelezo ,vingi vikimuonyesha Beyonce na kumalizika kwa maelezo yaliosema :Lemonade A world Permier event.
Na sasa mtengezaji  wa filamu  Matthew Fulks anadai kuwa kipande hicho kilinakili mojawapo ya kazi zake.
Fulks anadai kwamba kampuni ya muziki ya Sony ile ya Columbia Recordings pamoja na ile ya Beyonce Parkwood Entertainment zilijua kuhusu kazi yake kabla ya utengezaji wa Lemonade ulipoanza na kwamba walishawishiwa na kazi yake.
Anasema kuwa kipande hicho cha albamu ya Lemonade kinafanana na kile cha Palinoia ambayo ni kazi yake.
Anaongezea kuwa baadhi ya vitu vinavyofanana kati ya filamu hizo mbili ni pamoja na michoro katika ukuta,watu wenye macho mekundu na picha zilizopigwa katika ngazi pamoja na eneo la kuegesha magri chini ya nyumba.


ISIKILIZE HAPA REMIX YA BURGER MOVIE SELF YA BELLE9

Post a Comment
Powered by Blogger.