HIZI HAPA SABABU ZA KOCHA MPYA WA SIMBA KUCHELEWA KUSAINI MKATABA.

Sellas Tetteh Teivi.

Na Dorcas Safiel.

  BAADA ya kuwa na maswali mengi juu ya nini kinaichelewesha Simba kumtangaza Mghana, Sellas Tetteh kama kocha mpya wa klabu hiyo, sasa sababu halisi za kuchelewa huko zimejulikana.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Seetheafrica.com umebaini kuwa kocha huyo anasubiri mechi ya mwisho ya timu yake ya Sierra Leone kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (Afcon) 2017 dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa Septemba mwaka huu.
Sierra Leone iko Kundi I na timu za Sudan na Ivory Coast na inashika nafasi ya pili kwenye kundi lake ikiwa na pointi nne, pointi mmoja ya vinara Ivory Coast hivyo, Sellas bado anasubiri kuona kama ataweza kuipeleka Sierra Leone nchini Gabon kwa kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Ivory Coast.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Liberty Professionals, alikuwa anatarajiwa kutua nchini wiki iliyopita, lakini akaombwa kuendelea na Shirikisho la Soka la Sierra Leone amalizie pambano hilo dhidi ya Ivory Coast kabla ya kutua nchini huku pia wakiendelea kumshawishi aongeze mkataba wa kuifundisha nchi hiyo.

Inadaiwa kuwa tayari Simba imemfunga kwa mkataba wa miaka miwili kocha huyo anayeheshimika nchini Ghana, lakini hawezi kutua mapema nchini kutokana na kubanwa na mkataba wake na Sierra Leone.

Taarifa kutoka ndani ya Simba pia zinadai kuwa kocha Jackson Mayanja, amepewa jukumu la kuanza kuandaa programu ya kujiandaa na msimu mpya wakati timu hiyo ikiendelea kusubiri ujio wa Sellas ambaye atatua nchini baada ya mechi ya mwisho ya Sierra Leone ya kufuzu mataifa ya Afrika ya Kundi I dhidi ya Ivory Coast.
Post a Comment
Powered by Blogger.