Hizi Hapa Mpya TETEZI ZA USAJILI WA SOKA ULAYA SIKU YA IJUMAA.

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 10.06.2016.

Jamie Vardy hatoanza katika mechi ya England dhidi ya Urusi kwenye mchezo wa Euro 2016 siku ya Jumamosi, meneja Roy Hodgson akitarajiwa kuanza na Adam Lallana na Raheem Sterling
(Daily Mail, The Times, Telegraph, Sun, Mirror).


Wakati huohuo Vardy ana asilimia 80 ya kutosaini kwenda Arsenal na kusalia Leicester (Independent)
Nahodha wa Watford Troy Deeney anataka kujiunga na mabingwa Leicester City, lakini klabu yake imekataa dau la pauni milioni 20 kutoka kwa mabingwa hao (Daily Mirror).


Real Madrid wako tayari kuwapa Juventus kiungo wao Isco, 24, katika juhudi za kumsajili Paul Pogba, 23 (Daily Mail).


Lakini Manchester United watawapa Juventus beki Matteo Darmian, 26, katika jaribio lao la kumsajili Pogba (Sun).


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anasema bado kuna uwezekano wa yeye kuwa meneja wa Ufaransa siku zijazo (Bein Sports, via Daily Mirror) Manchester United wamemuulizia kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan, 27, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal (Daily Mail).


Jose Mourinho anataka kumrejesha Nani, 29, Old Trafford kutoka Fernabahce (DHA, via Talksport)
Real Madrid wameacha kumfuatilia kipa wa Manchester United David de Gea, 25. (Marca).


West Brom wanataka mshambuliaji wake Saido Berahino, 22, kutoondoka licha ya Tottenham na Stoke kumnyatia (Daily Mirror).


Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amemtaka mshambuliaji Mario Balotelli kuhudhuria mazoezi ya kabla ya kuanza msimu baada ya AC Milan kuamua kutomsajili (Gazzetta dello Sport).


Inter Milan watapanda dau kumtaka kiungo wa Manchester City Yaya Toure baada ya klabu hiyo kununuliwa na wawekezaji kutoka China (Manchester Evening News).


Beki Kalidou Koulibaly anayesakwa na Chelsea amesema "vilabu vikubwa" vinataka kumsajili baada ya mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake Napoli kusuasua (L'Equipe) mkataba wa beki wa Liverpool Kolo Toure, 35, unamalizika mwisho wa mwezi huu na huenda akahamia Monaco.(Daily Mail).


Manchester United wamemuajiri kocha mwenye mafanikio makubwa wa vijana chipukizi John Peacock ili afanye mabadiliko katika academy ya klabu hiyo (Sun).


Liverpool wameanza mazungumzo na kiungo Emre Can, 22, kuhusu mkataba wa muda mrefu (Guardian)
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.