Hivi Ndivyo Wanajeshi Wa AU Walivyokamatwa Nchini Somalia Kwa Kuuza Silaha.


Maafisa wa usalama wa Somalia wamewatia nguvuni wanajeshi watano wa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika pamoja na watu kumi wa asili ya kisomali kwa tuhuma za kuuza bidhaa za kijeshi.

Mkuu wa Polisi, Mohamed Sheikh Hassan Hamud, amesema wanajeshi hao wa AU,walipatika wakiwauuzia raia bidha za kijeshi ikiwemo,mafuta ya petrol,mikoba na vitu vya kuharibu vilipuzi.

Mohamed Sheikh aliwaambia wanahabari katika mji mkuu wa Mogadishu kuwa,wanajeshi hao watano walikua chini ya uangalizi kwa muda, na polisi wamekua wakifanya uchunguzi dhidi ya madai hayo.

Ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa kulinda amani wa AU, kukamatwa somalia yangu waanze kuhudumu nchini humo miaka tisa iliyopita.

Waziri wa usalama wa ndani wa Somalia Mohamed Sheikh,amedhibitisha kuwa wanajeshi hao walifanya biashara hiyo haramu akiongeza kuwa mienendo yao inaeleza ni kwa nini visa vya utovu wa usalama vinazidi kuongezeka Somalia.
Post a Comment
Powered by Blogger.