Hillary Clinton Aweka Rekodi Na Kuwa Mwanamke Wa Kwanza Marekani,Yeye Atoa Ujumbe Huu.

Hillary Clinton.
Bi Hillary Clinton amesema ameshinda uteuzi wa urais wa chama cha Democratic, kufuatia ushindi wake katika uteuzi wa mashinani katika jimbo ya New Jersey na pia uungwaji mkono unaotarajiwa kutoka kwa wajumbe maalum.
Bi Clinton sasa atakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuteuliwa na chama chochote kikuu nchini Marekani. Akiongea na wafuasi wake waliojawa na furaha, katika eneo la Brooklyn Bi Clinton amesema kuwa historia imeandikishwa nchini Marekani.
Bi Clinton amempongeza mpinzani wake Bernie Sanders kwa kuendesha kampeini kwa njia ya uadilifu, akisema ushindani wao uliimarisha mdahalo wa kisiasa nchini humo.
Aidha ameshutumu mgombea wa chama cha Republican na kumtaja kama mtu anayeendesha siasa za mgawanyiko na kuwa hafai kuwa rais wa Marekani.
Bernie Sanders hajakubali kushindwa na anatarajia kufanya vyema katika uteuzi wa mashindani katika jimbo la Carlifonia, ambalo halijatangaza matokeo yake na huenda akawashawishi wajumbe maalum wa chama hicho kumuunga mkono.
Post a Comment
Powered by Blogger.