Hii Hatari Russia Yadaiwa Kudukua Data Za Democrats Kuhusu Donald Trump.

Mrs.Wasserman Schultz.

Wadukuzi wa mitandao katika serikali ya Urusi waliingilia na kudukua kompyuta za kamati ya kimataifa ya Democrats ili kupata mikakati ya chama hicho ya kumpinga mgomea wa Republican Donald Trump.
Kompyuta hizo za DNC ziliingiliwa katika 'kisa kibaya' kulingana na mwenyekiti Debbie Wasseman Schultz.
Kampuni moja ya usalama wa mitandaoni tayari imepewa kazi ya kusaidia ,alisema ili kuwafurusha wadukuzi na kuimarisha usalama wa mtandao.
Hatahivyo Urusi imekana kutekeleza udukuzi huo.''Ninaondoa uwezekano wowote kwamba huenda serikali ya Urusi au vitengo vyake vilihusika na udukuzi huo'',alisema Dmitry Peskov msemaji wa Kermlin.
Post a Comment
Powered by Blogger.