HEKIMA ITUMIKE KUINUSURU AMANI UCHAGUZI WA YANGA.

HEKIMA ITUMIKE KUINUSURU AMANI UCHAGUZI WA YANGA.

Gumzo kubwa ktk michezo kila kukicha hasa kwa wapenda soka hapa nchini ni juu ya uchaguzi wa klabu kongwe hapa nchini Dar young Africa.
Gumzo linaletwa na mabishano kama siyo mashindano yaliyopo kati ya klabu na shirikisho la soka hapa nchini yaani TFF.
Sina muda wa kuchambua hoja za pande zote kwak├║wa wengi wamechangia katika hili na kikubwa kinachoendelea hivi sasa ni kumtafuta mchawi na kutengeneza bomu ambalo litakapolipuka litatuumiza sote na kutuacha na majuto kwa miaka mingi ijayo.
Najaribu kufikiria juu ya hiki kinachoendelea na ninapata swali ambalo nakosa jibu, je! Ni nani aliye nyuma ya sakata hili na anafaidikaje?
ANGALIZO: "panapokuwa na mgogoro kwenye klabu hizi mbili wapo wanaofaidika na migogoro hiyo."
Baraza la Michezo la Taifa "BMT" watabeba lawama zote kwa haya machafuko waliyoyatengeza. Katibu mkuu wa baraza hilo ndg Mohamed Kiganja, mara baada ya kuingia ofisini kufuatia uteuzi wake, alikuta viporo vya majukumu mbalimbali viliachwa bila utekelezaji kutoka kwa mtangulizi wake. Moja ya viporo hivyo ni uchaguzi wa Yanga ambao ulitakiwa kufanyika miaka miwili iliyopita na kwa ridhaa ya wanachama kupitia mkutano mkuu waliamua kuuongezea muda uongozi uliopo ili kupisha marekebisho ya katiba ya klabu kwa mujibu wa matakwa ya TFF chini ya mwongozo wa shirikisho la soka la dunia FIFA.
Kwa lugha nyepesi shirikisho la soka nchini "TFF" linajua kwa undani nini kimechelewesha uchaguzi Yanga.
Wakati mtendaji mpya ndg Kiganja anashughulikia baadhi ya viporo aliamua kukutana na wadau wa ngumi ili kuangalia njia bora ya kuendesha ngumi za kulipwa nchini na wakaja na mwafaka wa pamoja, nilitegemea angefanya hivyo hivyo kwa klabu ya Yanga, kwamba angekutana na uongozi uliopo madarakani chini ya bwn Yusuph Manji na kupata kiini cha kuchelewa kwa uchaguzi kisha watoke na mwafaka wa pamoja juu ya tarehe ya uchaguzi nk
Lakini kinyume chake ilitoka amri tena isiyo na mjadala kana kwamba klabu haina uongozi au kuna mpasuko na kwamba kuna wanachama wanaopiga kelele juu ya hilo.
Bila shaka uongozi uliopo upo kwa ridhaa ya mkutano mkuu wa wanachama ambacho ndicho chombo cha juu kabisa cha maamuzi katika klabu hiyo. Hivyo kufanya jambo lolote bila kushirikiana nao inatafsiriwa kama hujuma dhidi ya uongozi na klabu kwa ujumla.
Kasi yauchukuaji fomu mara baada ya tangazo la kamati ya uchaguzi ya TFF ilikuwa inatafsiri majibu ya wanachama wa Yanga dhidi ya hatua hiyo ya TFF.
Nilitegemea zaidi hatua zozote zinachokuliwa na baraza, shirikisho na klabu zije kama "zao" la mikutano na majadiliano ya pamoja.
Hebu tuchukue mfano wa shirikisho la soka duniani FIFA, popote panapotokea vurugu kwa mmoja wa wanachama wake hutuma wawakilishi wake, kufanya upatanisho na kuja na muafaka wa pamoja, kisha hutoa agizo la aidha kufanya uchaguzi au jambo lingine.
Baada ya hapo FIFA hutuma wasimamizi wa uchaguzi huo, lakini hili la kwetu baraza wanataka kutuaminisha kuwa uongozi wa Yanga hautaki kuitisha uchaguzi kinyume cha matakwa ya katiba tena bila ridhaa ya wanachama wake, au kuna vurugu zitokanazo na pande mbili zinazopingana hivy ni lazima uwepo upande huru kusimamia uchaguzi huo.
Kwa hali niionavyo sasa, namna uongozi uliopo unavyokubalika kwa wanachama, baraza na shirikisho vinaanda vurugu za karne ikiwa matakwa ya wengi yatasiginwa.
Jambo rahisi ni makubaliano kati ya pande zinazohusika, na amri ya baraza itekelezwe na Yanga wenyewe bila ya kupokwa haki na mamlaka yao.
Tuepuke vurugu zisizo na msingi kungali bado na mlango wa kufanya hvy ila tusikaribishe "majuto" kwa ubabe usio na faida, hekima itumike.


Imani K Mbaga.
 0717469593
Post a Comment
Powered by Blogger.