Haya Ndo Mambo 10 Serikali Imetangaza Kubana Matumizi Nchini Tanzania.  1. Kuhakikisha mikutano yote ikiwa ni pamoja na mikutano ya bodi, mafunzo na semina inatumia kumbi za Serikali na Taasisi za Umma;
  2. Kutoa kipaumbele kwa Taasisi za Umma katika kutoa huduma kwa Serikali kama vile bima, usafirishaji wa barua, mizigo na vifurushi, matangazo na usafiri;
  3. Kudhibiti matumizi ya umeme, simu na maji ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara;
  4. Kudhibiti ulipaji wa mishahara kwa watumishi ili kuepuka malipo yasiyostahili. Aidha, Serikali itaendelea kufanya sensa ya watumishi wote;
  5. Kudhibiti utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ili kuepuka utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wasio stahili;
  6. Kuendelea kufanya ununuzi wa magari kwa pamoja na bidhaa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupata unafuu wa bei;
  7. Kuendelea kudhibiti gharama za uendeshaji wa magari ikiwa ni pamoja na matengenezo, mafuta na vilainishi;
  8. Kupunguza na kuondoa matumizi yasiyo na tija katika maeneo mbalimbali ikiwemo maadhimisho na sherehe za kitaifa, matamasha, machapisho na safari za ndani na nje ya nchi zisizo na tija;
  9. Kuhimiza matumizi ya nakala laini (soft copy) za machapisho mbalimbali hususan yanayozidi kurasa 50 ili kupunguza gharama za uchapishaji na kutunza mazingira; na
  10. Kudhibiti matumizi ya Taasisi na Mashirika ya Umma yasiyowiana na majukumu yao ya msingi na yasiyo na tija.
Post a Comment
Powered by Blogger.