HAYA NDO MAAMUZI YA WEMA SEPETU KWA ZARI WA DIAMOND.MISS Tanzania 2006 na mmoja wa wacheza filamu mahiri wa kike nchini, Wema Sepetu, amesema kwamba anatamani mno kuonana na mke wa mkali wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’, Zari ili waweze kuzungumza kama anavyofanya kwa watu wengine.

Wema, binti anayetajwa kuwa na mvuto wa kipekee wa kimapenzi, anasema siku zote amekuwa akipenda kuwa na uhusiano mzuri na kila mtu, awe ni staa au mtu wa kawaida.

“Kuna watu wamekuwa wakilazimisha kunigombanisha na marafiki zangu, huwa sipendi kuwa na bifu na mtu yeyote…hata mke wa Diamond, Zari (Zarina Hassan), natamani kukutana naye hata leo na kubadilishana naye mawazo kuonyesha jinsi ambavyo sina bifu naye kama watu wanavyofikiria,” alisema Wema.

Wema mwenye sifa ya kufunguka kadiri anavyoweza, hata kwa mambo yake binafsi, alisema kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, anatamani kufanya kila jambo linaloonekana kuwa jema kwa jamii kama sehemu ya kutekeleza ipasavyo swaumu yake.

Wema amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond kabla ya wawili hao kuachana na mkali huyo wa Bongo Fleva kujikuta akinasa kwa Zari, mwanadada kutoka Uganda.

Bingwa
Post a Comment
Powered by Blogger.