Haya Ndo Maamuzi Ya Chama Cha Mafundi Simu Na TCRA.
CHAMA cha Mafundi Simu nchini kimesema hakitamfumbia macho fundi yeyote atakayehusika katika kuharibu mfumo wa rajisi za utambulisho katika simu baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) kuzima simu feki.

Akizungumza  wakati wa semina ya wadau wa mawasiliano kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani, Mwenyekiti wa chama hicho, Gwakisa Mwakatika alisema ni lazima kila fundi afuate taratibu na weledi wa kazi na kuacha kujihusisha na kuharibu mfumo wa rajisi za utambulisho na wizi.

Alisema semina hiyo iliyotolewa na TCRA itawasaidia wadau hao kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kutoa tahadhari kwa mafundi hao.Alisema mafundi kazi yao kubwa sio kurekebisha rajisi wanachokifanya ni kutengeneza simu zilizoharibika pekee, hivyo ni jukumu la kila fundi simu kuhakikisha anachokifanya na kurekebisha simu iliyoharibika.
Post a Comment
Powered by Blogger.