Haya Hapa Matokeo Ya COPA AMERICA,Marekani Yafanya Kufuru Ya Mabao Na Colombia Yatinga Robo Fainali.Michuano ya  Copa Amerika iliendelea tena Alfajiri  leo kwa  mechi mbili ambazo zimechezwa  Marekani wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Costa Rica.
Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Colombia na Paraguay na Colombia imeendeleza vimbi la Ushindi baada ya kushinda mabao 2-1na kutinga robo fainali kwa mechi ya kwanza waliwafunga Marekani mabao 2-0 hivyo kuwa timu ya kwanza kuingia hatua ya robo fainali.
Mechi za kesho ni Brazil atakwaana na Haiti na Equador wataminyana na Peru.


Huku bara la Afrika na Ulaya kwa ujumla limepatwa na msiba mkubwa mchezaji wa zamani wa Nigeria na baadaye akaja kuwa kocha wa Timu hiyo ya Super Eagles Stephen Okechukwu Chinedu Keshi ameiaga Dunia saa chache zilizopita.
Watu wake wa karibu wanasema hakuwa na tatizo lolote la afya lakini inadhaniwa amepatwa mshituko wa moyo.
Mwishoni mwa mwaka uliopita Keshi alimpoteza mkewe kutokana na saratani, nduguze wanasema huenda ameshindwa kuibeba hali hiyo ya kumkosa mkewe waliyedumu naye kwa miaka 35.
Post a Comment
Powered by Blogger.