Haya Hapa Matokeo Ya COPA AMERICA Kundi C,Uruguay Aibu Kwa Mexico.

Michuano ya Copa America iliendelea tena usiku wa leo nchini Marekan mechi mbili zilichezwa zikiwa katika kundi C, ambapo Mexico walicheza na Uruguay huku Mexico wakishinda mabao 3-1 na Jamaica wamefungwa bao 1-0 na Venezuela.
 Mexico walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 4 baada ya beki wa Uruguay Alvaro Pereira kujifunga na katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza Matias Vecino wa Uruguay alizawadiwa kadi nyekundu baada ya mwanzo kupata ya njano hadi mapumziko Mexico walikuwa wanaongoza bao 1-0.
Alvaro Pereira.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Luis Suarez na Cavani wakikosa mabao ya wazi mnamo dakika ya 73 Andres Guardado wa Mexico alitolewa nje kwa kadi nyekundu na katika dakika ya 73 beki kisiki na Nahodha Diego Godin aliisawazishia Uruguay bao.
Diego Godin.
Watu wakiamini kuwa mchezo huu utaisha kwa sare mnamo dakika ya 85 Mexico walipata bao la pili kupitia kwa Rafael Marguez.
Rafael Marguez.
Dakika ya 90 Mexico walipata bao la tatu na ushindi kwao na kuendelea kuongoza kundi kupitia kwa Hector Moreno.
Hector Moreno.
Matokeo mengine ni Venezuela imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamaica bao la Venezuela lilifungwa dakika ya 15 na mshambuliaji hatari Josef Martinez kwa shuti kali.
Josef Martinez.


Post a Comment
Powered by Blogger.