HAYA HAPA MAAMUZI YA CHADEMA KUHUSU MKUTANO MKUU WA CCM JULAI 23.

9Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamelitaka Jeshi la Polisi nchini kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika Julai 23, 2016 mkoani Dodoma.
CCM inatarajia kufanya mkutano huo mwezi ujao, ukiwa na lengo moja la kumkabidhi Rais Magufuli kiti cha uenyekiti wa chama hicho.
CHADEMA kimelitaka jeshi la polisi, kama lilivyozui mahafali ya CHASO mkoani Dodoma na Kilimanjaro kwa kile walichodai kuwa intelijensia yao imebaini kuwa kutakuwa na vurugu basi hivyo hivyo wauzuie na wa CCM kwani vyote ni vyama vya siasa vilivyokatazwa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara.
Aidha akizungumza, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana CHADEMA, Julius Mwita amesema kuwa kama jeshi hilo halitauzuia mkutano huo, basi wao kwa kutumia nguvu ya umma watauzuia.
Msimamo huo umeungwa mkono na viongozi wengine wakuu wa chama akiwamo Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salim Mwalim.
Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano yote na maandamano ya vyama vya siasa kwa madai ya kusababisha vurugu na kuwashawishi wananchi kutotii sheria. Hii ni baada ya vyama vya upinzani kutaka kufanya mikutano nchi nzima kuelezea kutoridhishwa na mwenendo wa demokrasia ndani ya Bunge na nchini kwa ujumla.
Post a Comment
Powered by Blogger.