HAWA NDIYO MO BEJAIA WANAOPAMBANA NA YUSSUPH MANJI.

Kikosi cha Mo Bejaia.

HAWA NDIYO MO BEJAIA.

Wajuzi wa mambo wanasema silaha ya kwanza ya kupambana na adui yako ni kumjua vilivyo na kumfanyia tathmini ya kutosha ili uweze kujua jinsi ya kupambana naye.
Bila shaka kuelekea michezo ya hatua ya nane bora, maadui wakubwa wa Yanga ni Mo Bejaia, Tp Mazembe na Medeama.
Siku ya Jumapili Dar Young Africans watajitupa ktk dimba la Stade de I'unite Maghrebine huko mjini Bejaia nchini Algeria kupepetana na wenyeji wao Mo Bejaia ya huko. Sasa swali kubwa hapa ni Mo Bejaia ni nani hasa?
Timu ya Mo Bejaia ilianzishwa mwaka 1954 na inapatika mjini Bejaia umbali wa kama saa mbili hv kwa njia ya barabara kutokea mji mkuu wa Algeria.
Uwanja wa nyumbani wa timu hiyo unaitwa Stade de I'unite Maghrebine na una uwezo wa kuhimili mashabiki wasiopungua elfu kumi na mbili (12000) hv.
Mo Bejaia wamewahi kuwa mabingwa wa kombe la Ageria mwaka 2015 ukiwa ubingwa pekee mkubwa waliowahi kuupata ngazi ya kitaifa. 


TAKWIMU ZA MSIMU ULIOPITA.
Bila shaka takwimu ndiyo njia ya kisasa ya kufanya tathmini ya jambo, hvy takwimu ktk msimu uliopita kwa Mo Bejaia ni kama ifuatavyo.
Kwa upande wa ligi ya nyumbani kwao wamecheza mechi 30, kati ya hizo 15 nyumbani na 15 ugenini.
Walishinda jumla ya mechi 11 kati ya hizo mechi 8 walishinda wakiwa uwanja wa nyumbani na 3 ugenini.
Walitoka sare mechi 11 ambapo mechi 6 walitoka sare nyumbani na 5 ugenini.
Walipoteza michezo 8 na kati ya hiyo 1 walipoteza wakiwa nyumbani na 7 ugenini.
Wamefunga magoli 33 kati ya hayo 17 wakiwa nyumbani na 16 wakiwa ugenini. Lkn pia wamefungwa magoli 23 kati ya hayo 7 walifungwa wakiwa nyumbani na 16 wakiwa ugenini.
Walijikusanyia alama 44 kati ya hizo alama 30 walizipata nyumbani na 14 pekee walizipata ugenini.
Hawakuruhusu wavu wao kuguswa yaani "clean sheet" 12 na kati ya hizo 8 wakiwa nyumbani na 4 wakiwa ugenini.
Walishindwa kufunga katika michezo 14 kati ya hiyo 5 ni ya nyumbani na 9 ya ugenini.
Ushindi mkubwa waliowahi kuupata ni 5-1, na kipigo kikubwa ni 2-0.
24% ya magolí yao yalipatikana kati ya dakika ya 45-60.
Kwa upande wa michuano ya kimataifa timu ya Mo Bejaia hadi kufikia sasa imefunga jumla ya magoli 6 na kufungwa 5, ambapo magoli yote 6 waliyofúnga waliyàfúñgà wakiwà nyumbani huku yale waliyofungwa 2 walifungwa wakiwa nyumbani na 3 wakiwa ugenini
Kwa jumla takwimu zinaonyesha wakiwa nyumbani wanakuwa bora zaidi licha ya kwamba inaonekana pia wanajilinda kwa nguvu na kutumia nafasi chache wanazozipata.
Dar Young Africans wanaonekana kutopata matokeo mazuri sana ugenini licha ya kucheza vizuri zaidi ugenini kuliko nyumbani.
Hata hivyo hatua hii ni ya makundi kwa mtindo wa ligi na siyo mtoano hivyo tunatarajia mabadiliko kadhaa katika mbinu, mfumo na hata uchezaji kulingana na malengo.
Nitaendelea kukuletea dondoo muhimu kadri siku zinavyokwenda.


Kila la heri Dar Young Africans.


Imani K Mbaga.


0717469593

Post a Comment
Powered by Blogger.