Hatimaye TFF Yabariki Uchaguzi Wa Yanga Na Pia Ikitoa Tamko.

Jengo-la-TFF1
Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi leo alikutana na secretariat ya Yanga chini ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake madarakani Bw. Clement Sanga na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit kwa ajili ya kujadili mustakabali wa uchaguzi wa Yanga ambao uliingia katika mvutano na TFF pamoja na BMT.
Rais wa TFF Jamal Malinzi

Maamuzi yaliyotoka ni kwamba, uchaguzi wa Yanga umebarikiwa kuendelea kama ulivyopangwa na kamati ya uchaguzi ya Yanga kwamba utafanyika June 11, 2016 chini ya uangalizi wa kamati ya uchaguzi ya TFF.

Wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo ambao walichukua fomu TFF, kikao kimeamua kiwarudishe kamati ya uchaguzi ya Yanga kuendelea na taratibu zilizopo za uchaguzi endapo wanakidhi vigezo vya uchaguzi vya kamati ya uchaguzi ya Yanga.


Post a Comment
Powered by Blogger.