Hatimaye Inter Milana Yauzwa Kwa Suning Toka China.


Kampuni kubwa zaidi ya uundaji wa vifaa vya elektoniki ya China, itanunua asilimia 70 ya umiliki wa klabu ya soka ya Italia, Inter Milan.
Suning italipa dola milioni 360, ilihali tajiri mkubwa nchini Indonesia Erick Thohir atasalia na asilimia zake 30.
Mwenyekiti wa Suning, Zhang Jindong ameutaja ununuzi huo kama hatua kubwa mno kwa soka nchini Uchina, huku akitabiri kuwa China itakuwa nyumba ya pili kwa Klabu ya Inter Milan.
Rais wa China Xi Jin-ping ameshuhudia ukuaji mkubwa wa mtizamo wa China kuhusiana na kombe la Dunia huku akitoa wito kwa timu ya soka ya taifa hilo kushinda kombe la Dunia mnamo mwaka wa 2050.
Post a Comment
Powered by Blogger.