Hatimaye Bandari Ya Libya Yakombolewa Kutoka Kwa Islamic State.


Vikosi vya Libya vinavyoegemea serikali ya muungano mjini Tripoli vinasema kuwa vimeichukua bandari ya mji wa sirte, kufuatia makabiliano makali baina yao na wapiganaji wa Islamic state.

Msemaji wa kikosi hicho jenerali Muhammad al-Ghusri anasema viongozi wakuu wa Islamic State wametorokea jangwani, akiongeza kuwa wapiganaji wengi wa Islamic State wamezingirwa mjini Sirte na kuwa makabiliano yanaendelea.
Vita vya kuukomboa mji wa Sirte kutoka kwa wapiganaji hao ikiwa ndio ngome yao muhimu nje ya Iraq na Syria vilianza mwezi uliopita.
Vikosi hivyo vinavyounga mkono serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli vilianza harakati za kuukomboa mji huo mwezi uliopita.
Post a Comment
Powered by Blogger.